Thursday 27 November 2014

UBORA WA UTU WAKO

UBORA WA UTU WAKO

...Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa Neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo(Yakobo 1:22-24)

     Mstari wetu wa ufunguzi haujadili juu ya taswira, kwa maana ya umbo la nje au mwonekano wa mtu ajitizamaye katika kioo, bali ni "namna" au "aina" ya mtu. Mtendaji wa Neno hasahau "namna" yake alivyo; kiwango cha ubora wa utu wake.
    Utaelewa hilo vema endapo utasoma kuanzia mstari wa kumi na nane; inasema "Kwa kupenda Kwake Mwenyewe Alituzaa sisi kwa Neno la Kweli, tuwe kama limbuko la viumbe Vyake"(Yakobo 1:18).
     Mungu Alituzaa sisi kwa Neno la kweli; Ambalo ni, Injili ya Kristo, ili tuwe namna au aina ya uzao wa kwanza wa viumbe Wake. Hii ni ya kustaajabisha! Maana ya uzao wa kwanza ni nini? Inamaanisha wa kwanza na wa ubora wa juu kabisa wa viumbe wa Mungu.
     Ulipozaliwa mara ya pili, ukawa na aina ya ubora mpya wa maisha-maisha ya Mungu. 2 Wakorintho 5:17 inasema, " Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya." Kama kiumbe kipya ndani ya Kristo Yesu, wewe ni ukamilifu wa uzuri, na ubora wa juu kabisa wa kila kitu ambacho Mungu ameumba. Una nguvu dhidi ya shetani.
     Hivyo, Mkristo anaposema, "Nahitaji ukombozi dhidi ya shetani," ni kwa sababu amesahau "namna" na "aina" ya utu wake. Utahitaji vipi ukombozi dhidi ya shetani wakati wewe una nguvu zaidi yake?
     Biblia inasema umeketi pamoja na Kristo katika mbingu, juu zaidi ya mamlaka na nguvu zote. Upo katika mahala pa mamlaka ya juu kabisa ndani ya Kristo Yesu, juu sana ya shetani na kila kitu kinachohusiana naye.
     Fahamu ubora wa utu wako. Ndiyo maana tunakuletea Neno la Mungu kila siku kwa njia tofauti, kukupa nuru ya jinsi ulivyo ndani ya Kristo.

     Maombi
Baba Mpendwa, Nakushukuru kwa kunifanya wa kwanza na wa ubora wa juu katika vyote ulivyoviumba. Mimi ni utimilifu wa uzuri, wa mtindo wa ubora wa juu kabisa. Maisha yangu ni udhihirisho wa utukufu na ukuu wako; naonyesha ukamilifu wako na kudhihirisha hekima yako sura mbali mbali kwa ulimwengu, katika jina Lake Yesu. Amina

Soma Zaidi:
Warumi 6:4
Basi tulizikwa pamoja Naye kwa njia ya ubatizo katika mauti Yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

Waefeso 2:10
Maana tu kazi Yake(kazi ya mikono yake), tuliumbwa tena katika Kristo Yesu, tuenende katika kazi njema, ambazo tokea awali Mungu aliziandaa ili tuenende kwazo.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Waebrania 12:14-29
Ezekieli 13-15

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Yohana 3:1-12
Ezekieli 47.

HAKIKISHA UNASEMA SEHEMU YA "MAOMBI" AU "UKIRI" KWA SAUTI, USISEME MOYONI, KUNA UMUHIMU MKUBWA KATIKA KUSEMA.

No comments:

Post a Comment