Sunday 9 November 2014

AINA TATU ZA IMANI


Yakobo 2:14-26

UTANGULIZI
1.Imani ni kitu muhimu sana katika maisha ya mkristo.
a.Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Ebra 11:6
“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”
b.Mkristo anaokolewa kwa imani. Efeso 2:8
8Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
c.Mkristo anapaswa kuishi kwa imani. 2 Korintho 5:7

Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.

d.Jambo lolote tulifanyalo pasipo imani linaelezwa kuwa ni dhambi. Rumi 14:23
Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
2.Ni muhimu kutambua kuwa kuna aina tofauti za imani, lakini pamoja na hayo kuna imani moja tu ya kweli. “Imani iokoayo.”
3.Katika Yakobo 2:14-26 tunaona Yakobo akieleza aina tofauti za imani na anakazia kwenye imani itendayo kazi ya kuokoa roho.
(Tukianza na Yakobo 2:14-17 tunaona aina ya kwanza ya imani ambayo tunaweza kusema ni imani iliyokufa.)
14Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? 15Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? 17Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
AIMANI ILIYOKUFA (14-17)
IJINSI ILIVYO
1.Hubadili matendo kwa maneno.
a.Watu walio na imani hii huwa na sifa zifuatazo:
(1)Wanajua misamiati mizuri kwa maombi; pia wanajua mafundisho sahihi.
(2)Wanaweza kunukuu mistari ya Biblia kwa ufasaha zaidi.
b.Tatizo ni kwamba mwenendo wao hauendani na kile wanachokisema.
2.Imani hii ni imani ya ufahamu tu.
a.Iko kwenye mawazo ya mtu, mtu anajua mafundisho yote ya wokovu.
b.Lakini pamoja na kujua hayo mtu huyo hatii kile Mungu anachokiagiza wala hamtumainii Yesu katika wokovu wake.
c.Mkristo anaijua lakini haitendei kazi ile kweli.
IIJE IMANI HII INAWEZA KUOKOA?
1Hapana! Katika mistari mitatu Yakob 2: 17,20 na 26 Yakobo amesisitiza kuwa imani bila matendo imekufa.
2Tamko lolote la Imani lisiloleta mabadiliko katika maisha wala lisiloleta kazi njema ni tamko la uongo. Na hapo imani imekufa.
3Imani iliyokufa ni imani ya uongo inamwongoza mtu kwenye tumaini la uongo la uzima wa milele.
IIIJE TUNAYO IMANI ILIYOKUFA?
1Tunaweza kuwa nayo iwapo mwenendo wetu hauendani na maneno tunayosema.
2Tunaweza kuwa nayo iwapo kzi tuzifanyazo ziko kinyume na tunahubiri.
(Wapendwa yatupasa kuwa makini na imani ya kweny mawazo tu. Mana mtu mmoja alisema hakuna mtu ajaye kwa Yesu akawa kama alivyokuwa.)
Aina ya pili ya imani iliyoelezewa na yakobo ni…

BIMANI YA MASHETANI
IHata mashetani yanayo imani.
1Yanaamini katika Mungu(Si miungu bali ni Mungu)
2Yanaamini hata katika uungu wa Kristo. Mk 3:11-12
11Na pepo wachafu, kila walipomwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu. 12Akawakataza sana, wasimdhihirishe.
3.Si hivyo mapepo yanamini kuwepo na sehemu ya hukumu. Luka 8:31

Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.
4.Na zaidi mapepo yanaamini kuwa Yesu atakuwa Hakimu. Matayo 8:28-29

28Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. 29Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?

IIJINSI IMANI YA MASHETANI ILIVYO
Tumeona kuwa mtu mwenye imani iliyokufa huguswa kwenye ufahamu tu.
Mashetani yana guswa katika hisia zao. (kumbuka kuwa huamini na kutetemeka)
Hii imani iko juu zaidi ya imani iliyokufa. Inahusisha ufahamu na hisia.

IIIJE IMANI YA NAMNA HII INAWEZA KUOKOA?
1Hapana imani hii inaweza kuwemo ufahamuni mwa mtu na ikawemo moyoni mwake lakini mtu huyo akapotea milele.
2Imani ya kweli iokoayo inahusisha kitu zaidi, kitu zaidi ya kile kinachoweza kuonekana; mabadiliko katika maisha. Yakobo 2:18
18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
3Kuwa mkristo kunahusisha mambo mawili kumtumainia Kristo na kuishi kwa ajili ya Kristo.
a.Kwanza unapokea uzima.
b.Unadhihirisha uzima.

IVJE TUNAYO IMANI YA MASHETANI
1Tunaweza kuwa nayo iwapo tunaamini tu katika mambo sahihi na tunaishia kwenye hisia tu.
2Tunaweza kuwa na imani ya mashetani iwapo:
a.Kiufahamu tunakubali mafundisho sahihi.
b.Tunasisimuka kimazoea wakati wa ibada.
(Kwa hiyo Yakobo ameweka wazi kuwa aina hizi za imani kamwe haziwezi kuokoa; imani iliyokufa na imani ya mashetani. Yakobo pia akaendelea kuelezea kuhusu imani itendayo kazi ni imani pekee iokoayo.

CIMANI ITENDAYO KAZI (Yakobo 2:20-26)
20Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? 21Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? 22Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale. 23Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. 24Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake. 25Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? 26Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

AJE HII NI IMANI YA NAMNA GANI?

1Mahali pengine Biblia inatuambia kuwa imani msingi wake ni Neno la Mungu Rumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
2Imani itendayo kazi inamhusisha mtu mzima
a.Imani iliyokufa inahusisha ufahamu tu.
b.Imani ya mashetani inahusisha ufahamu na hisia.
c.Imani itendayo kazi inahusisha ufahamu, hisia na utashi.
(1)Ufahamu ni katika kuelewa kweli.
(2)Moyo ni kwa ajili ya shauku na kufurahi katika neno.
(3)Na utashi ni kwa ajili ya kutendea kazi kweli.
3Imani ya kweli, iokoayo huongoza kwenye matendo.
a.Si ya ufahamu tu.
b.Si ya hisia.
c.Ni imani itupelekayo kuwa na utii katika kufanya kazi njema.
BILI KUFAFANUA YAKOBO ANATUPA MFANO WA ABRAHAM NA RAHABU
1. Katika hawa tunaona kuwa:
a.Abraham alikuwa na baba wa wayahudi; Rahab alikuwa mmataifa.
b.Abrahamu alikuwa mcha Mungu; Rahabu alikuwa mwenye dhambi kahaba.
c.Abrahamu alikuwa rafiki wa Mungu lakini Rahabu alikuwa upande wa maadui wa Mungu.
2Je hawa wawili walikuwa na nini cha kuwafananisha? Wote walionyesha imani iokoayo kwa Mungu.
a.Abrahamu alionyesha imani yake kwa kazi zake. Yakobo 2:20-24
20Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? 21Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? 22Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale. 23Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. 24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.

b.Rahabu alionyesha imani yake kwa matendo yake. Yakobo 2:25-26
25Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? 26Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

3Kwa hiyo katika vifungu hivi tunajifunza kuwa:
a.Imani bila matendo imekufa. Yakobo 2: 20, 26
b.Imani peke yake haiwezi kumhesabia haki mtu. Yakobo 2:24
c.Imani kamilifu lazima iwe na matendo Yakobo 2:22
HITIMISHO
1Ni muhimu kila mwamini achunguze moyo na maisha yake na ahakikishe kuwa anayo imani iokoayo ambayo ni imani itendayo kazi.
2Shetani ni mdanganyifu mkuu na moja ya mbinu yake kuu ni kuiga…..
a.Anaweza kumshawishi mtu kuwa imani ya uongo ni ya kweli…na kwamba yule mtu anazo nguvu za kiroho.
3Yafuatayo ni maswali unayoweza kujiuliza katika kuichunguza imani yako.
a.Je kuna wakati nilijikugundua mwenyewe kuwa mimi ni mwenye dhambi na nikazikubali dhambi kwangu mwenyewe na kwa Mungu?
b.Je kuna wakati moyo wangu ulinisukuma niepuke ghadhabu ijayo. Je ni jitihada zipi nimefanya kuhusu dhambi zangu?
c.Je ni kweli naelewa injili kuwa kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zangu?
d.Je nilitubu dhambi kwa dhati na kuchukua uamuzi wa kuziacha? Je ninachukia dhambi na kumcha Mungu?
e.Je namtumania Kristo peke yake?
f.Je kuna mabadiliko katika maisha yangu? Je ninaendelea kutenda mema?
g.Je nina shauku ya kukua? Ninaweza kuwaambia wengine kuwa niko na Kristo?
h.Je ninafurahia ushirika na wapendwa?

2 comments:

  1. Real nimepata jambo jipya hapo.
    Mungu akubariki pia nitafanya citation ya somo lako

    ReplyDelete