Saturday 23 January 2016

NAMNA YA KUWATAMBUA MANABII WA UONGO.

Bwana Yesu alishatuonya tujihadhari na manabii wa uongo na tena akawafananisha na mbwa mwitu wakali waliovaa ngozi ya kondoo (Math 7:15-23). Yesu alibainisha wazi kuwa namna pekee ya kuwatambua ni kuyachunguza matunda yao..Lakini mtume Petro amerahisisha zaidi kwa kufafanua tabia zao ktk 2Pet 2:1-22.,Nazo ni...

{1} Wanaigiza kwa werevu na uzushi wa kupoteza watu..yaani manabii hawa huingiza mafundisho ya uongo kwa ustadi wa hali ya juu kiasi kwamba ni ngumu kugundua usipokuwa makini. (2Pet 2:1b Watakaoingia kwa werevu, uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijitetea uharibifu usiokawia)
{2} Watu wengi wanaomsikiliza watamfuata na ufisadi wake..na mara nyingi si ajabu kukuta wafuari wao wana tabia kama za manabii wao (2Pet 2:2 Na wengi watafuata ufisadi wao, na kwa hao njia ya kweli itatukanwa).
{3} Wanajipatia faida binafsi kutoka kwa wafuasi wao...Yaani unakuta mwongo akiwahadaa wafuasi wake na kujipatia fedha nyingi na kuwa tajiri mkubwa huku wafuasi wake wanabaki wakiwa maskini wa kutupwa (2 Pet 2:3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa, ambao hukumu yao tangu zamani haikawii wala uvunjifu wao hausinzii.)
{4} Wanapenda maisha ya anasa kupindukia..yani hatumii gari zaidi ya 1 year...(2Pet2:13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa, wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi.)
{5} Hawanaga hofu na dhambi...yani dhambi kwao ni kitu simple tu hasa uzinzi tena pengine wameonywa na kuonywa ila bado wanaendelea na maovu yao huku wakiwahubiria wafuasi wao na kusimama madhabahuni bila aibu...(2Pet2:14a Wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi,)
{6} Wanazihadaa roho zisizo imara..(2Pet2:14b Wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana,)..Tena manabii hawa wa uongo ni kama visima visivyo na maji..yani ukienda kwao ukitazamia kupata neno la uzima ujue imekula kwako..utaambulia mapokeo tu..(2Pet2:17 Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambamo weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.)
{7) Ni waongo na wenye kiburi...Utakuta nabii wa uongo akiwahadaa waumini wake kwa kuwa watoe kiasi fulani cha pesa na kuwaahidi maisha mazuri ya utajiri wa muda mfupi akitumia njia ambazo Yesu hakufundisha..(2Pet2:18 Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwaadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu.)
THE TRUTH CAN NOT BE HIDDEN!.

Somo hili limeandikwa na Eliapenda Mremi

No comments:

Post a Comment