Thursday 27 November 2014

MUUJIZA WA UPENDO WAKE

MUUJIZA WA UPENDO WAKE.

Na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu Tuliyepewa sisi(Warumi 5:5).

     Kila mara ninapo waza na kulitafakari Neno la Mungu na kuona ukuu wa Bwana, nastaajabishwa kwa kutambua kuwa Aliweka kabisa katika moyo wa mwanadamu, kiumbe Wake Mwenyewe, kule kumpenda. Ni muujiza wa kushangaza. Sijui kama ulishawahi kufikiria ukweli kwamba Alikuumba.
     Unajua, ni rahisi kwetu kuhusiana Naye bila kutambua mara moja, kuwa tunahusiana kabisa na Aliyetuumba: vyote tulivyo, na Anafahamu kila kitu kuhusu sisi. Ukuu Wake ni kupita maelezo.
     Kwa hiyo inanyenyekeza mno, na inastaajabisha ufahamu, kufikiri kuwa Aliweka ndani ya mioyo yetu kumfuata na kumpenda. Kufikiri kuwa Alifanya iwezekane sisi kumjua, na kutaka kumjua zaidi, kama sehemu ya kazi Yake ndani yetu, ni ukweli unaoshangaza sana.
     Unapo waza kuhusu wale wasiomfahamu, fikiria umebahatika kiasi gani kwamba unamjua, si eti kwa sababu ulipata kumgundua, bali kwa sababu Aliweka ndani ya moyo wako kumjua. Bora zaidi kuliko yote ni kuwa, sasa Amekufanya kuwa mshirika Wake katika kuwavuna waliopotea.
     Angeweza kuwafanya wamjue Yeye bila kukuhusisha, kwa sababu Yeye ni Mungu; Ana nguvu zote na Anaweza kufanya vitu vyote. Lakini, Alituchagua kuwa sehemu ya kazi Yake ya kuwaleta wengine katika wokovu; ni muujiza! Ni heshima.

    Maombi
Baba Mpendwa, nina furaha kiasi gani kujua kwamba, si tu kuwa Ulinipenda kwa upendo wa milele, bali Uliweka pia katika moyo wangu kukupenda, Bwana wangu na Muumbaji. Moyo wangu wasujudu katika kukuabudu, kwa ukuu Wako, na kwa heshima na ufahari wa kukujua, kukupenda, na kukutumikia. Nitashangilia na kuimba juu ya ukuu na upendo Wako siku zangu zote, katika jina Lake Yesu. Amina.

Somo Zaidi:
Zaburi 8:4-6 Mtu ni kitu gani hata ukamkumbuka, na mwanadamu hata umtembelee? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemuweka juu ya kazi za mikono Yako; ukavitia vitu vyote chini ya miguu yake.

Waefeso 1:5 Akiwa Alikwishatangulia kutuchagua, katika kufanywa wanawe ndani ya Yesu Kristo,  sawa sawa na mapenzi Yake."AMP"

1 Yohana 3:1 Tazama, ni pendo la namna gani Alilotupatia Baba, ya kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua Yeye.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yakobo 3:14-4:1-12
Ezekieli 22-23

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Yohana 5:1-21
Danieli 5-6

No comments:

Post a Comment