Thursday 27 November 2014

NI KATIKA ROHO...SIO UFAHAMU

NI KATIKA ROHO...SIYO UFAHAMU.

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo Yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli(Yohana 4:24)

     1 Wakorintho 2:14 inasema," Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni." Hii ni kwa sababu ukristo ni zaidi ya hisia! Ukosefu wa uelewa wa ukweli huu husababisha wengi kuchanganyikiwa katika kutembea kwao kiimani. Mungu huwasiliana na roho yako, si ufahamu wako. Imani huzalishwa katika roho na si katika ufahamu; ni mwitikio wa roho yako katika Neno la Mungu. Haihusiani kabisa na hisia zako.
     Hisia zetu hazikuumbwa ili kumhisi Mungu; Tunatembea Naye kutoka katika roho zetu; tunamtumikia kwa roho zetu, na kuelewa uhalisia wa mambo ya kiroho kwa kupitia roho. Fahamu zetu hazikuundwa kwa kazi hiyo; roho zetu tu ndizo zinaweza kuhusiana na Mungu. Kisha, kulingana na huo uhusiano, tunazipanga fahamu zetu kutokana na roho ili ziendane nayo, na kuongoza hisia zetu kutimiza kusudi letu.
     Hii inamaanisha, mwonekano tunaouonesha nje wakati wote unategemea hali ya roho zetu- jinsi tulivyo ndani.
     Ndiyo maana tunamuhitaji Roho Mtakatifu kutuongoza kwa kutokea ndani. Yeye pekee Ndiye Awezaye kufika ndani kabisa ya asili ya mwanadamu na kufanya mabadiliko ambayo Mungu huyataka kwetu- mabadiliko katika ukuaji na maendeleo-kutoka kiwango kimoja cha utukufu hadi kingine. Yeye pekee huweza kuongoza fahamu zetu kuwaza kwa kumwelekea Mungu, kufikiri kama Mungu, na kufikiri kutoka kwa Mungu.

  Maombi
Baba Mpendwa, nakushukuru kwa kuniongoza kwa Roho wako, kufikiri kama Wewe, na kuona mambo kwa mtazamo wako, na siyo tu katika mtazamo wa kibinadamu. Kadri nitembeavyo katika nuru ya Neno Lako, napata uzoefu wa ukuaji wa kipekee kutoka utukufu hadi utukufu, katika jina la Yesu. Amina.

Somo Zaidi:
Warumi 12:2
Wala msifwatishe namna ya dunia hii; bali mkageuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Waefeso 4:23-24
..na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu upya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yakobo 1
Ezekieli 17-19

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Yohana 4:1-14
Danieli 1-2.

No comments:

Post a Comment