Nimeitoa mahali naamini itakusaidia kijana
Andiko la Msingi ni Mithali 5:1-20
"Mungu ndiye aliyewaumba mtu mume na mtu mke, akawaweka bustanini ili
wamtumikie. Mungu akamuumba mwanadamu na kumpa viungo mbalimbali katika
mwili. Akawapa wanadamu maungo maalumu kwa ajili ya tendo la ndoa na
kisha akaliweka tendo la ndoa kuwa takatifu, tena la halali kwa wanandoa
tu, tena hasa wale waliounganishwa na yeye."
Sasa katika kizazi cha
leo tunaona watu wengi hasa vijana ambao bado hawajaoana (kwa maana ya
kuwa wanandoa) vijana hao wanafanya tendo hilo la ndoa (ngono) tena kwa
uchafu usio wa kawaida, wanafanya kwa kuzidi mipaka ambayo Mungu amempa
mwanadamu, maana yake wanatumia isivyo (mis-use) maumbile/ maungo ambayo
Mungu amewapa.
Soma warumi 1:24-27. Sasa wao wanapofanya haya
hawajui kwamba kuna hasara kubwa wanayoipata na wao wanafikiri ndio
wanakwenda na dunia. Lengo la ujumbe huu ni kukueleza hasara za kufanya
tendo la ndoa kabla ya ndoa nazo ni;
(1)Ni dhambi
Kufanya
ngono kabla ya ndoa ni dhambi na warumi 6:23a inasema mshahara wa dhambi
ni mauti; na pia katika Ezekiel anasema Roho itendayo dhambi ndiyo
itakayokufa, hivyo kwa sababu hiyo hicho kitendo kitakusababishia kifo
cha kimwili na kisha utahukumiwa tu na mwisho kutupwa jehnamu.
(2)Kuwashibisha wengine nguvu zako
Mithali 5:10 Tendo la ndoa ni tendo linalohitaji mtu atumie nguvu,
hivyo kadri mtu (hasa mwanume) anapofanya mara kwa mara anajipotezea
nguvu zake anawashibisha wengine nguvu zake na hivyo dhoruba itamkuta
katika ndoa yake pindi atakapooa kwa sababu hatakua na nguvu tena kama
awali.
(3)Utavunjiwa heshima
Mithali 5:7, Siku zote yule
unayefanya naye tendo la ndoa kwanza atakuona wewe ni mpumpavu kwa
sababu anajua afanyaye tendo hilo hana akili kabisa (mithali 6:32) kwa
hivyo atakudharau, zaidi atakutangaza kwa wengine na wewe mwenyewe pindi
utapooa au kuolewa kwa kuwa nguvu zako uliwashibisha wengine basi
utavunjiwa heshima na huyo mwenzi wako.
(4)Unafanya jambo litakaloiangamiza nafsi yako
Mithali 6:32. Nafsi kwa kiyunani inaitwa Psuche, ndani yake kuna hisia,
akili na maamuzi ya mtu. Hivyo kuiangamiza nafsi yako ni kuangamiza
future yako na mipango yako uliyokuwa umejiwekea ya mbele.
(5)Unajitengenezea majeraha na fedheha maishani
Mithali 6:33. Sikiliza katika ngono unaweza ukapata kilema cha maisha,
na magonjwa ya hatari kama vile kaswende, ukimwi n.k. Haya magonjwa
yatapelekea nyama na mwili wako kuangamia utashindwa kufikia malengo
uliyojipagia, utabakia kujuta tu na watu watakufanyia fedheha na wakati
huo upo kitandani hujiwezi.
(6)Kuwapa wengine miaka yako
Mithali 5:9 , Uchunguzi chunguzi unaonyesha kwa mtu anayependelea
kufanya ngono mara kwa mara hasa anapoanza kabla ya ndoa mara nyingi
hawezi kuishi kwa muda mrefu si hivyo tu lakini pia tumeona mara nyingi
vijana wakijiua/wakiuana /wakifa kwa ajili ya mapenzi, wengine wanaugua
hadi wanakufa wadogo na kupatwa na magonjwa mabaya, na hivyo muda
waliostahili waishi hapa duniani na hivyo wanakuwa wamewapa wengine
miaka yao.
(7)Kuvamiwa na maroho machafu
Katika kufanya
ngono, wengine wanaenda hadi kwa waganga wa kienyeji na wachawi na huko
wengine wanapewa madawa ya ajabu ambayo yanapelekea kuwamiwa na mapepo
ya ajabu, na wengine kwa kupenda ngono wamefanya ngono na majini bila
wao kujua na tayari yamesha wamiliki na hawaji watatokaje kwenye kifungo
hicho.
Mimi nimekuonyesha hasara zile za kibiblia tu, sasa zipo za
kijamii, kitaifa, kifamilia nk. Naamini baada ya kuwa umesoma ujumbe
huu, kama bado unafanya ngono basi utabadili tabia yako na kuacha ngono
mpaka wakati utakapo fika na kama haujaokoka nakusihi uokoke ili Yesu
akupe nguvu za kushinda hiyo dhambi.
Bwana Mungu akulinde na kukutunza.
Somo hili limeanadaliwa na kuandikwa na dada Mary Muna
No comments:
Post a Comment