Thursday 27 November 2014

UKUU WA MUNGU

Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye?Asema yeye aliye Mtakatifu. Inueni macho yenu juu, mkaone;ni nani aliyeziumba hizi; (Isaya 40:25-26a)
Ukuu wa Mungu Wetu
Hivi, unaposikia Mungu ni mkuu huwa unamfikiria kuwa yukoje? Ni kweli hatuwezi kujua kwa hakika Mungu yukoje, lakini angalau kuna mambo kadhaa ambayo yeye mwenyewe anatueleza kuhusu jinsi alivyo.
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? (Isaya 66:1). Hebu tazama juu mbinguni kisha piga picha ya hicho kiti kinachoanzia mbinguni hadi duniani

Nabii Isaya Mungu anatupa changamoto ya kuinua macho yetu, tutazame ‘hizi’, yaani nyota, kisha tutafakari ni nani aliyeziweka pale juu. Ulimwengu huu tuliomo ni mpana mno mno kuliko ambavyo tunaweza kupata maneno ya kuelezea au kuliko ambavyo akili zetu zinaweza kuelewa!
BWANA asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyotenda, asema BWANA. (Yeremia 31:37). ‘Mbingu’ hapa inamaanisha anga. Anachosema Mungu hapa ni kuwa haiwezekani kwa mwanadamu kupima mapana na marefu kamili ya mbingu maana ni pana sana sana!

Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari kupimwa;ndivyo nitakavyoongeza wazao wa Daudi...(Yeremia 33:22). ‘Jeshi la mbinguni’ linalotajwa hapa ni nyota. Mungu anasema kuwa hakuna mwanadamu anayeweza kuzihesabu nyota zote, maana ni nyingi mno!

No comments:

Post a Comment