Thursday 27 November 2014

UBORA WA UTU WAKO

UBORA WA UTU WAKO

...Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa Neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo(Yakobo 1:22-24)

     Mstari wetu wa ufunguzi haujadili juu ya taswira, kwa maana ya umbo la nje au mwonekano wa mtu ajitizamaye katika kioo, bali ni "namna" au "aina" ya mtu. Mtendaji wa Neno hasahau "namna" yake alivyo; kiwango cha ubora wa utu wake.
    Utaelewa hilo vema endapo utasoma kuanzia mstari wa kumi na nane; inasema "Kwa kupenda Kwake Mwenyewe Alituzaa sisi kwa Neno la Kweli, tuwe kama limbuko la viumbe Vyake"(Yakobo 1:18).
     Mungu Alituzaa sisi kwa Neno la kweli; Ambalo ni, Injili ya Kristo, ili tuwe namna au aina ya uzao wa kwanza wa viumbe Wake. Hii ni ya kustaajabisha! Maana ya uzao wa kwanza ni nini? Inamaanisha wa kwanza na wa ubora wa juu kabisa wa viumbe wa Mungu.
     Ulipozaliwa mara ya pili, ukawa na aina ya ubora mpya wa maisha-maisha ya Mungu. 2 Wakorintho 5:17 inasema, " Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya." Kama kiumbe kipya ndani ya Kristo Yesu, wewe ni ukamilifu wa uzuri, na ubora wa juu kabisa wa kila kitu ambacho Mungu ameumba. Una nguvu dhidi ya shetani.
     Hivyo, Mkristo anaposema, "Nahitaji ukombozi dhidi ya shetani," ni kwa sababu amesahau "namna" na "aina" ya utu wake. Utahitaji vipi ukombozi dhidi ya shetani wakati wewe una nguvu zaidi yake?
     Biblia inasema umeketi pamoja na Kristo katika mbingu, juu zaidi ya mamlaka na nguvu zote. Upo katika mahala pa mamlaka ya juu kabisa ndani ya Kristo Yesu, juu sana ya shetani na kila kitu kinachohusiana naye.
     Fahamu ubora wa utu wako. Ndiyo maana tunakuletea Neno la Mungu kila siku kwa njia tofauti, kukupa nuru ya jinsi ulivyo ndani ya Kristo.

     Maombi
Baba Mpendwa, Nakushukuru kwa kunifanya wa kwanza na wa ubora wa juu katika vyote ulivyoviumba. Mimi ni utimilifu wa uzuri, wa mtindo wa ubora wa juu kabisa. Maisha yangu ni udhihirisho wa utukufu na ukuu wako; naonyesha ukamilifu wako na kudhihirisha hekima yako sura mbali mbali kwa ulimwengu, katika jina Lake Yesu. Amina

Soma Zaidi:
Warumi 6:4
Basi tulizikwa pamoja Naye kwa njia ya ubatizo katika mauti Yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

Waefeso 2:10
Maana tu kazi Yake(kazi ya mikono yake), tuliumbwa tena katika Kristo Yesu, tuenende katika kazi njema, ambazo tokea awali Mungu aliziandaa ili tuenende kwazo.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Waebrania 12:14-29
Ezekieli 13-15

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Yohana 3:1-12
Ezekieli 47.

HAKIKISHA UNASEMA SEHEMU YA "MAOMBI" AU "UKIRI" KWA SAUTI, USISEME MOYONI, KUNA UMUHIMU MKUBWA KATIKA KUSEMA.

NI KATIKA ROHO...SIO UFAHAMU

NI KATIKA ROHO...SIYO UFAHAMU.

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo Yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli(Yohana 4:24)

     1 Wakorintho 2:14 inasema," Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni." Hii ni kwa sababu ukristo ni zaidi ya hisia! Ukosefu wa uelewa wa ukweli huu husababisha wengi kuchanganyikiwa katika kutembea kwao kiimani. Mungu huwasiliana na roho yako, si ufahamu wako. Imani huzalishwa katika roho na si katika ufahamu; ni mwitikio wa roho yako katika Neno la Mungu. Haihusiani kabisa na hisia zako.
     Hisia zetu hazikuumbwa ili kumhisi Mungu; Tunatembea Naye kutoka katika roho zetu; tunamtumikia kwa roho zetu, na kuelewa uhalisia wa mambo ya kiroho kwa kupitia roho. Fahamu zetu hazikuundwa kwa kazi hiyo; roho zetu tu ndizo zinaweza kuhusiana na Mungu. Kisha, kulingana na huo uhusiano, tunazipanga fahamu zetu kutokana na roho ili ziendane nayo, na kuongoza hisia zetu kutimiza kusudi letu.
     Hii inamaanisha, mwonekano tunaouonesha nje wakati wote unategemea hali ya roho zetu- jinsi tulivyo ndani.
     Ndiyo maana tunamuhitaji Roho Mtakatifu kutuongoza kwa kutokea ndani. Yeye pekee Ndiye Awezaye kufika ndani kabisa ya asili ya mwanadamu na kufanya mabadiliko ambayo Mungu huyataka kwetu- mabadiliko katika ukuaji na maendeleo-kutoka kiwango kimoja cha utukufu hadi kingine. Yeye pekee huweza kuongoza fahamu zetu kuwaza kwa kumwelekea Mungu, kufikiri kama Mungu, na kufikiri kutoka kwa Mungu.

  Maombi
Baba Mpendwa, nakushukuru kwa kuniongoza kwa Roho wako, kufikiri kama Wewe, na kuona mambo kwa mtazamo wako, na siyo tu katika mtazamo wa kibinadamu. Kadri nitembeavyo katika nuru ya Neno Lako, napata uzoefu wa ukuaji wa kipekee kutoka utukufu hadi utukufu, katika jina la Yesu. Amina.

Somo Zaidi:
Warumi 12:2
Wala msifwatishe namna ya dunia hii; bali mkageuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Waefeso 4:23-24
..na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu upya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yakobo 1
Ezekieli 17-19

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Yohana 4:1-14
Danieli 1-2.

VAA SILAHA ZA VITA MKRISTO

Silaha hutengenezwa wakati wa amani japo hutumika wakati wavita
Wakristo wakati wa amani hawaombi ila mambo yakigeuka kidogo hufunga nakuomba
Wakati unazama si wakati wakujifunza kuogelea
Unapaswa kujifunza kabla
Fanya maazimio na Mungu wako siku za amani
Simama kwenye zamu yako kikamilifu
Mtafute Mungu kwa bidii Mith 8:17
Andaa na uvae silaha sasa Efe 6:11
Kumbusha wapendwa japo 15 maana sms za utani unatuma sana
Leo tuma hii takatifu,
Mungu akubariki..

NGUVU YA KUTOA PEPO

Yesu Akamkemea, Akisema, fumba kinywa,  umtoke. Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka( Marko 1:25-26).

     Marko 16:17-18 inasema, "ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina Langu watatoa pepo...." Kila Mkristo anao uwezo wa kuwatoa pepo! Sio swala la kwamba "una nguvu" kiasi gani au jinsi gani upo "kiroho" ; cha muhimu ni kuwa Yesu Amekupa mamlaka Yake; unatembea katika jina Lake.
    Shetani hana haki ya kuendesha mambo katika maisha yako, au nyumbani mwako au katika maisha ya wale uwapendao. Tumia mamlaka yako katika Kristo dhidi yake.
     Unaweza kuwatoa pepo siku yoyote, muda wowote na mahala popote, kwa kutumia jina la Yesu tu. Usijadiliane naye; mtoe!
     Unaweza ukajiuliza. "Nitajuaje kuwa pepo ametoka ninapomkemea?" Hilo ni rahisi. Yesu Alisema, unapowaambia pepo watoke, hutoka. Neno Lake Linakamilisha hilo. Kazi yako ni kumkemea pepo atoke, na jukumu lake pepo ni kutii.
     Ingawa, wakati mwingine pepo hujionesha na kulia kwa sauti pindi wanapomtoka yule mtu unayewatoa kwake. Mfano ni kama tulivyosoma katika mstari wetu wa ufunguzi. Pia tunaona tukio kama hilo katika matendo 8:6-8 pale Filipo alipomuhubiri Kristo kwa watu: "...pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu..."
    Hivyo, katika kutoa pepo, roho waovu huweza kupiga yowe na kelele kwa kuteseka pindi wanapotoka; na kisha badiliko la wazi kwa wale ambao pepo wamewatoka hujionesha kuwa kuna tofauti.
     Hata hivyo, haijalishi pepo wamepiga yowe au kelele wakati ulipowakemea; cha muhimu ni kile Yesu Alichokisema,"...kwa jina Langu mtatoa pepo..."( Marko 16:17). Huo ndiyo uhalisia, na unapaswa kuwa ndiyo msingi wa imani yako. Hivyo, unapowakemea pepo, wanakuwa hawana chaguo lolote- zaidi ya kukimbia.

   Maombi
Baba Mpendwa, nakushukuru kwa mamlaka Uliyonipa ya kukemea pepo katika jina la Yesu. Shetani na wafuasi wake hawana nafasi katika nyumba yangu, mwili, kazi na kipato changu. Natumia mamlaka yangu katika Kristo kuwaweka pale wanapostahili- chini ya miguu yangu. Katika jina la Yesu. Amina.

Somo Zaidi:
Luka 10:18-19  Akawaambia, Nilimwona shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, Nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na ng'e, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.

Matendo 16:16-18  Ikawa tulipo kuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema watu hawa ni watumishi wa Mungu Aliye juu, wenye kuwahubiria Njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo Akakasirika, akageuka akamwambia yule pepo, nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yakobo 2-3:1-13
Ezekieli 20-21

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Yohana 4:14-21
Danieli 3-4.

UKUU WA MUNGU

Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye?Asema yeye aliye Mtakatifu. Inueni macho yenu juu, mkaone;ni nani aliyeziumba hizi; (Isaya 40:25-26a)
Ukuu wa Mungu Wetu
Hivi, unaposikia Mungu ni mkuu huwa unamfikiria kuwa yukoje? Ni kweli hatuwezi kujua kwa hakika Mungu yukoje, lakini angalau kuna mambo kadhaa ambayo yeye mwenyewe anatueleza kuhusu jinsi alivyo.
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? (Isaya 66:1). Hebu tazama juu mbinguni kisha piga picha ya hicho kiti kinachoanzia mbinguni hadi duniani

Nabii Isaya Mungu anatupa changamoto ya kuinua macho yetu, tutazame ‘hizi’, yaani nyota, kisha tutafakari ni nani aliyeziweka pale juu. Ulimwengu huu tuliomo ni mpana mno mno kuliko ambavyo tunaweza kupata maneno ya kuelezea au kuliko ambavyo akili zetu zinaweza kuelewa!
BWANA asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyotenda, asema BWANA. (Yeremia 31:37). ‘Mbingu’ hapa inamaanisha anga. Anachosema Mungu hapa ni kuwa haiwezekani kwa mwanadamu kupima mapana na marefu kamili ya mbingu maana ni pana sana sana!

Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari kupimwa;ndivyo nitakavyoongeza wazao wa Daudi...(Yeremia 33:22). ‘Jeshi la mbinguni’ linalotajwa hapa ni nyota. Mungu anasema kuwa hakuna mwanadamu anayeweza kuzihesabu nyota zote, maana ni nyingi mno!

MUUJIZA WA UPENDO WAKE

MUUJIZA WA UPENDO WAKE.

Na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu Tuliyepewa sisi(Warumi 5:5).

     Kila mara ninapo waza na kulitafakari Neno la Mungu na kuona ukuu wa Bwana, nastaajabishwa kwa kutambua kuwa Aliweka kabisa katika moyo wa mwanadamu, kiumbe Wake Mwenyewe, kule kumpenda. Ni muujiza wa kushangaza. Sijui kama ulishawahi kufikiria ukweli kwamba Alikuumba.
     Unajua, ni rahisi kwetu kuhusiana Naye bila kutambua mara moja, kuwa tunahusiana kabisa na Aliyetuumba: vyote tulivyo, na Anafahamu kila kitu kuhusu sisi. Ukuu Wake ni kupita maelezo.
     Kwa hiyo inanyenyekeza mno, na inastaajabisha ufahamu, kufikiri kuwa Aliweka ndani ya mioyo yetu kumfuata na kumpenda. Kufikiri kuwa Alifanya iwezekane sisi kumjua, na kutaka kumjua zaidi, kama sehemu ya kazi Yake ndani yetu, ni ukweli unaoshangaza sana.
     Unapo waza kuhusu wale wasiomfahamu, fikiria umebahatika kiasi gani kwamba unamjua, si eti kwa sababu ulipata kumgundua, bali kwa sababu Aliweka ndani ya moyo wako kumjua. Bora zaidi kuliko yote ni kuwa, sasa Amekufanya kuwa mshirika Wake katika kuwavuna waliopotea.
     Angeweza kuwafanya wamjue Yeye bila kukuhusisha, kwa sababu Yeye ni Mungu; Ana nguvu zote na Anaweza kufanya vitu vyote. Lakini, Alituchagua kuwa sehemu ya kazi Yake ya kuwaleta wengine katika wokovu; ni muujiza! Ni heshima.

    Maombi
Baba Mpendwa, nina furaha kiasi gani kujua kwamba, si tu kuwa Ulinipenda kwa upendo wa milele, bali Uliweka pia katika moyo wangu kukupenda, Bwana wangu na Muumbaji. Moyo wangu wasujudu katika kukuabudu, kwa ukuu Wako, na kwa heshima na ufahari wa kukujua, kukupenda, na kukutumikia. Nitashangilia na kuimba juu ya ukuu na upendo Wako siku zangu zote, katika jina Lake Yesu. Amina.

Somo Zaidi:
Zaburi 8:4-6 Mtu ni kitu gani hata ukamkumbuka, na mwanadamu hata umtembelee? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemuweka juu ya kazi za mikono Yako; ukavitia vitu vyote chini ya miguu yake.

Waefeso 1:5 Akiwa Alikwishatangulia kutuchagua, katika kufanywa wanawe ndani ya Yesu Kristo,  sawa sawa na mapenzi Yake."AMP"

1 Yohana 3:1 Tazama, ni pendo la namna gani Alilotupatia Baba, ya kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua Yeye.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yakobo 3:14-4:1-12
Ezekieli 22-23

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Yohana 5:1-21
Danieli 5-6

WAKUFANANA NAYE

bible ya kiswahili inasema wakufanana naye
ya kizungu inasema Wakufanana"FIT FOR HIM"
"FIT"
nini kinatakiwa kifit ule ubavu ulioondolewa wakati wa kuurudisha lazma ufit pale
ukirudisha oversize lazma ilete shida
ukirudisha undersize napo lazma ulete shida
kama ubavu wako ulikuwa umekamilika pasi na shida ukirudisha wenye shida lazma utateseka huo ubavu utageuka mwiba

naaa hakuna mwanadamu aujuaye ubavu wake isipokuwa Mungu pekee
ndiposa yatupasa kumsubiria
kwann twamsubiria
maana yeye ndiye aijuaye size ya kila mmoja
naa ndiye ajuaye majira muafaka ya kuurudisha ubavu ama kichwa
twamsubiria kwa namna gani
kwa kudumu katika maombi

naa wale wajuao kumsubiria Bwana miyoyoni mwao kunakuwa kumejaa neno ni si sura za mabint ama vijana ambao angependa awe nao

unaposogea kutafuta jawabu kwa Baba kumuhusu mwenza wako
hakikisha huna mtu moyoni ambaye unamfikiria nenda mbele za Bwana mtupu ili urudi na KITU

kingine usipende kuiga et kisa ulimsikia mch.wako akisema
yeye almpata mama mch.kwa kuweka unyasi kichwani ili mwanamke atakaye utoa awe ndiye ndiposa mama akautoa naa ndo akampata nawe ukaiga
what if akaja mbibi akatoa huo unyasi

naa isije ikawa wewe ni mtumishi ukakazana kuwafuatilia mabint wasio na utume ndani yao
baibo inasema ""akamfanyia msaidiz ""
sasa ukimchukua asiye na utume atakusaidiaje
wewe wataka kwenda kuomba yeye anataka mmege mkate
hata kiasi akijui

haaa bint mwenza ma Hb wanguvu kutoka kwa Mungu hawapatikani kwa kuwaekea mitego
mana mitego mingine si mitego ni chakula cha mtegwaji
tulia jtunze mngoje Mungu kwa wakati wake atakupa

yamkini walalama umri umeenda ila believe my words umri siyo obstacle kwa Mungu
mana hakika anajua wakati huu akikupa hutoweza kumtunza wala kumsaidia so its better kutulia na
kumwacha Mungu akutengeneze kwaajili
ya mweshimiwa

mi najua moja nalo nmelishika
kwamba aliye wangu mume wangu mupenz
hakuna anayeweza kumchukua katka ulimwengu huu
mana nmeandikiwa fulani ni wangu
haijalish yupo wapi najua naye ananijua naa ataiona njia ya kunijia
naa kaz yangu n kumtengenezea njia afike kwa maombi tu

AINA MBILI ZA HATIMA

AINA MBILI ZA HATMA.

Na wale aliyowachagua tangu asili, hao Akawaita; na wale Aliowaita, hao Akawahesabia haki, hao Aliowahesabia haki Akawatukuza( Warumi 8:30)

     Kuna hatma mbili kwa kila mwanadamu. Kuna hatma ya kidunia na hatma ya KiUngu. Hatma ya kidunia huongozwa na vigezo kama vile familia uliyozaliwa, nchi uliyozaliwa, watu unaohusiana nao, taarifa unazozipokea au elimu n.k. Hayo yote yana matokeo katika hatma yako ya kidunia.
     Kwa mfano, kuna wale ambao ni matajiri, si kwa mafanikio yao wenyewe, bali kwa sababu ya familia walizozaliwa. Hiyo ndiyo hatma yao ya kidunia.
     Hatma ya kidunia hata hivyo, haiondoi kuhusika kwa mkono wa Mungu wa kiUngu wenye uweza; Ana uhusika wa ujumla katika ulimwengu. Ulimwengu ni mali yake. Lakini kuna baadhi katika ulimwengu huu ni viumbe wake, huku wengine ni wana wake. Analo kusudi jema kwa viumbe Wake wote- kila mmoja duniani- bali kipekee(maalumu) zaidi, Anayo hatma ya kiUngu kwa wana Wake- kila aliyezaliwa mara ya pili.
     Hatma ya kiUngu kwa kila mwanadamu huanza tu pindi anapozaliwa mara ya pili. Pale ndipo Mungu huwa Baba yako naye huanza kukuongoza. Pale ndipo Humtumtuma Roho Mtakatifu kuishi ndani yako na kukuongoza. Sasa Roho Mtakatifu huweka makazi ndani ya moyo wako.
    Wewe ni wa tofauti na ulimwengu. Kama Yesu Alivyosema katika Yohana 15:19, "...bali Mimi Nilliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia." Kila aliyezaliwa mara ya pili si wa ulimwegu huu. Umechaguliwa toka ulimwengu huu na Yesu. Ana alama zake kwako.
      Utajuaje kama mtu anatimiza hatma yake ya kidunia au ya kiUngu? Ni rahisi: nani hujitwalia utukufu katika maisha yake? Katika mambo afanyayo, ni nani hupokea heshima? Ni nani hupokea sifa? Ni nguvu ya nani inayomuwezesha kufanya afanyayo? Anaishi kwa ajili ya nani? Kama majibu yote yataonesha kuwa ni BWANA, basi hiyo ni hatma ya kiUngu, kwa mujibu wa biblia.

    Ukiri

Maisha yangu ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Nilizaliwa ili kumpa heshima, na kuonesha ubora Wake na ukamilifu katika ulimwengu huu. Hekima Yako, neema, na haki vinaonekana, kadri unavyodhihirisha ladha ya ujuzi Wako kupitia mimi kila mahali; hii ni hatma yangu: kuishi kwa ajili ya Yeye Aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.

Somo Zaidi:
2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.

Yeremia 1:5 Kabla sikakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Waefeso 1:11 Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawa sawa na kusudi Lake Yeye, Ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi Yake.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
1 Petro 1:1-21
Ezekieli 27-28

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
3 Yohana
Danieli 9-10.

UKISOMA HII UNAWEZA KUJENGEKA KIIMANI

UKIPATA NAFASI YA KUSOMA STORY HII SOMA INAWEZA IKAKUJENGA KIIMANI.

Ni siku nyingi kidogo, mwaka 1979, lakini ni tukio ambalo liliniuma sana. Ilikuwa vigumu sana kulisahau na lilinifanya nijiulize, inakuwaje Mungu anakuwa mkatili kiasi kile. Lakini bila shaka ilikuwa ni wakati ule wa ufahamu mdogo. Hivi sasa ninafahamu mengi na hasa baada ya kujifunza maarifa haya ya utambuzi.Ilikuwa ni mwaka 1979 nikiwa nasafiri kutokea Dar es salaam kwenda Arusha. Sijui ilikuwaje, lakini ilitokea. Tuliondoka Dar es salaam saa 12.30 jioni. Wakati ule mabasi yalikuwa yakisafiri jioni na usiku, sio kama siku hizi.Nilikuwa ninakwenda Arusha kwenye usaili kwa ajili ya ajira, nikiwa ndio kwanza nimemaliza kidato cha nne. Niliajiriwa moja kwa moja serikalini, kwani siku zile ajira zilikuwa ni za kumwaga. Hata hivyo sikuridhishwa na kazi niliyokuwa nafanya, hivyo niliomba kazi kwenye kampuni moja kule Arusha na niliitwa kwa usaili.Tulifika mji unaoitwa Korogwe ambao wakati ule ulikuwa ndio mji maarufu kwa hoteli zake katika barabara yote ya Segera hadi Moshi na Arusha. Tulipofika Korogwe basi letu lilisimama kwa ajili ya abiria kupata chakula. Niliingia kwenye hoteli moja ambayo nakumbuka hadi leo kwamba ilikuwa ikiitwa Bamboo. Niliagiza chakula na kula haraka kutokana na muda mfupi wa kula uliotolewa na wenye basi la TTBS ambalo ndilo nililosafiri nalo.Wakati wa kulipa ndipo niliposhangaa na kuogopa. Niliingiza mkono mifukoni na kukuta kwamba sikuwa na hela. Nilianza kubabaika na mwenye hoteli alisema hawezi kukubali ujinga huo, "Abiria wengine wahuni bwana, anakula na kujifanya kaibiwa, ukikubaliana nao kila siku hasara tu" Mwenye hoteli alisema kwa kudhamiria hasa.Kulizuka zogo kubwa, huku mwenye hoteli akisema ni lazima anipeleke polisi. Ni kweli alimtuma mmoja wa watumishi wake kwenda kituo cha polisi ili nishughulikiwe..Hapo Hotelini kulikuwa na bwana mmoja aliyekuwa amekaa pembeni na mkewe na watoto wao wakila. Yule bwana alipoona vile alimtuma mhudumu mmoja aniite. Niliondoka pale kaunta nilipokuwa nabembeleza na kuja kwa yule bwana.Alikuwa ni kijana mtu mzima kidogo, mwenye miaka kama 50 hivi. Nilimsalimia na aliitikia, nilimsalimia mkewe pia. Yule bwana aliniuliza kisa cha vurugu ile na nilimsimulia. Aliniuliza sasa huko Arusha ningeishi vipi wakati wa usaili wakati nimeibiwa fedha zote na ningerudi vipi Dar. Nilimwambia nilikuwa napanga namna ya kurudi Dar, kama huko polisi ningeaminika.Kama mzaha vile yule bwana aliniambia kuwa angenipa fedha za kutumia huko Arusha na nikirudi Dar nimrudishie fedha zake. Nakumbuka alinipa shilingi 90 kwa ahadi kwamba nikirudi Dar nimpelekee fedha zake ofisini kwake. Alinielekeza ofisini kwake, mtaa wa Nkuruma na kuniambia kuwa ameamua kunisaidia kwa sababu kila binadamu anahitaji msaada wa mwingine na maisha haya ni mzunguko. Nilimshukuru na kuondoka kukimbilia basini. Basi lilikuwa linanisubiri mimi tu. Nilipanda ndani ya basi na abiria wengine walinipa pole. Tuliondoka Korogwe, lakini haikuchukua muda basi letu lilipata tatizo la pancha ya gurudumu moja la mbele. Ilibidi tuegeshe pembeni ili litengenezwe. Baada ya matengenezo, tuliondoka kuendelea na safari yetu.Karibu na mji wa Same kwenye saa saba usiku, basi letu lilisimama ghafla. Abiria walisimama ndani ya basi na kulizuka aina ya kusukumana. Huko nje kulikuwa na ajali. Abiria tulishuka haraka na wengine huko chini walishaanza kupiga mayowe, hasa wanawake. Niliposhuka niliona gari ndogo nyeusi ikiwa imebondeka sana na hapo kando kulikuwa na maiti wawili.Nilijua ni maiti kwa sababu walikuwa wamefunikwa gubigubi. Halafu kulikuwa na katoto kalikokuwa kanalia sana kakiwa kamefungwa kanga kichwani. Tumwahishe huyu mtoto hapo Same hospitali ameumia, ingawa sio sana. Nilikatazama kale katoto ka kiume kenye umri wa miaka kama mitatu. alikuwa ameumia kwenye paji la uso, lakini kalikuwa hai. Bila shaka wale walikuwa ni wazazi wake, kalikuwa yatima tayari. Machozi yalinitoka.Baada ya kupata msaada na askari wa usalama barabarani kuchukua maiti wale tulipanda basini kuendelea na safari yetu. Kale katoto kalichukuliwa na jamaa fulani waliokuwa na Land Rover ya serikali kukimbizwa hospitalini. Ndani ya Basi mazungumzo yalikuwa ni kuhusu ajali ile tu, hadi tunafika Arusha. Tulichelewa sana kufika Arusha kwani tulifika kwenye saa tano asubuhi, badala ya saa mbili .Nililala kwenye hoteli rahisi na kufanya usaili kesho yake. Ni hiyo kesho, baada ya usaili niliponunua gazeti ambapo nilipata mshtuko mkubwa ajabu. Kumbe wale watu wawili waliokufa kwenye ajali ile ya Same walikuwa ni yule bwana aliyenisaidia hela na mkewe. Yule mtoto wao ndiye aliyeokoka. Niligundua hilo baada ya kusoma jina lake na jina la kampuni aliponiambia nimpelekee fedha zake nikirudi Dar, pamoja na picha yake, mke na mtoto. Nililia sana, kama mtoto.Nillishindwa kujua ni kwa nini afe. Nilijiuliza ni nani sasa angemlea mtoto yule? Yalikuwa ni maswali yasiyo na majibu na pengine maswali ya kijinga pia.Nilijua kwamba nilikuwa na deni, deni la shilingi tisini. Kwa wakati ule shilingi tisini zilikuwa ni sawa na shilingi laki moja za sasa.Kwa mara ya kwanza sasa nilijiuliza ni kwa nini marehemu yule aliniamini nakuamua kunipa fedha zile. Sikupata jibu.Nilikata kipande kile cha gazeti la kingereza kilichokuwa na habari ile. Nilichukuwa kipande hicho na kukiweka kwenye Diary yangu. Deni, Ningelipa vipi deni la watu? Nilijikuta nikipiga magoti na kuomba mungu anipe uwezo wa kuja kulilipa deni la mtu yule mwema kwa njia yoyote. 'Mungu naomba uje uniwezeshe kulilipa deni la marehemu kwa sura na namna ujuavyo wewe. Nataka kulilipa deni hili ili nami niwe nimemfanyia jambo marehemu,' niliomba. Nilirejea Dar siku hiyo hiyo.Kwa sababu ya mambo mengi na hasa baada ya matokeo ya usaili ule kuwa mbaya kwangu, nilijikuta nikiwa na mambo mengi na kusahau haraka sana kuhusu mtu yule aliyenisaidia mbaye ni marehemu. Nilifanikiwa hata hivyo kupata nafasi ya kusoma Chuo cha Saruji na baadae chuo cha ufundi na hatimaye nilibahatika kwenda nchini Uingereza. Mwaka 1991 nilianza shughuli zangu.Ilikuwa ni mwaka 1995 nikiwa ofisini kwangu pale lilipokuwa jengo Nasaco ambalo liliungua mwaka 1996, ambapo lilijengwa upya na kubadilishwa jina na kuitwa Water Front. Nikiwa nafanya kazi zangu niliambiwa na sekratari wangu kwamba kulikuwa na kijana aliyekuwa anataka kuniona. Nilimuuliza ni kijana gani, akasema hamjui. Nilimwambia amruhusu aingie. Kijana huyo aliingia ofisini. Alikuwa ni kijana mdogo wa umri miaka kama 17 au 18 hivi, mweupe mrefu kidogo. Alikuwa amevaa bora liende , yaani hovyohovyo huku afya yake ikiwa hairidhishi sana.Nilimkaribisha ilimradi basi tu, kwani niliona atanipotezea bure muda wangu. Ni lazima niwe mkweli kwamba sikuwa mtu mwenye huruma sana na nilikuwa naamini sana katika watu wenye pesa au majina. Nilimuuliza, "nikusaidie nini kijana na ukifanya haraka nitashukuru maana nina kikao baada ya muda mfupi". Nilisema na sikuwa na kikao chochote , lakini nilitaka tu aondoke haraka."Samahani mzee, nilikuwa na shida...nimefukuzwa shule na sina tena mtu wakunisaidia kwa sababu ...nime..niko ..kidato cha pili na hivyo tu natafuta tu kama atatokea mtu....Nilimkatisha. "Sikiliza kijana. Kama huna jambo lingine la kusema, ni bora ukaniacha nifanye kazi. Hivi unafikiri kama nikiamua kumsaidia kila mtu aliyefukuzwa shule si nitarudi kwetu kwa miguu! Nenda Wizara ya Elimu waambie..Kwanza wazazi wako wanafanya kitu gani, kwa nini washindwe ...Kwa nini walikupeleka shule ya kulipia kama hawana uwezo, wanataka sifa?""Hapana wazazi wangu walikufa na ninasoma shule ya serikali. Nimekosa mahitaji ya msingi na nauli ya kwendea shule. Nasoma shule ya Kwiro, Morogoro. Shangazi ndiye anayenisomesha, naye ana kansa na hivi sasa hata kazi hafanyi..," Alianza kulia. Huruma fulani ilinijia na nilijiambia, kama ni nauli tu na matumizi, kwa nini nisiwe mwema, angalau kwa mara moja tu. "Baba na mama walifariki lini?" Niliuliza nikijua kwamba, watakuwa wamekufa kwa ukimwi, maana kipindi kile ndipo fasheni ya ukimwi ilipoanza, ambapo kila anayekufa huhesabiwa kwamba kafa kwa ukimwi."Walikufa kwa ajali nilipokuwa mdogo sana, nilipokuwa na miaka mitatu. Ndio shangazi yangu akanichukua na kunilea hadi sasa anakufa kwa kansa." Yule kijana alilia zaidi. Naomba nikwambie wewe msomaji unayesoma hapa kwamba, kuna nguvu fulani na sasa naamini kwamba ziko nyingi ambazo huwa zinaongoza maisha yetu bila sisi kujua.Kitu fulani kilinipiga akilini paaa! Nilijikuta namuuliza yuel kijana. "Kwa nini umeamua kuja kwangu, ni nani alikuelekeza hapa na wazazi wako walikufa mwaka gani na wapi?"Yule kijana alisema, "Nimeona nijaribu tu kwa mtu yeyote ambaye anaweza kunisaidia, na ndio nimejikuta nikiingia hapa, sijui....sikutumwa na mtu. Wazazi wangu walikufa mwaka 1979 huko Same na mimi wanasema nilikuwa kwenye ajali, nikaokoka. Niliumia tu hapa." Alishika kwenye kovu juu ya paji lake la uso.Nilihisi kitu fulani kikipanda tumboni na kuja kifuani halafi niliona kama vile nimebanwa na kushindwa kupumua. "Baba yako alikuwa anaitwa nani?" "Alikuwa anaitwa Siame..Cosmas Siame.." Niliinuka ghafla hadi yule kijana alishtuka . Nilikwenda kwenye kabati langu mle ofisini na kuchakura kwenye droo moja na kutoka na diary. Mikono ikinitetemeka, nilitoa kipande cha gazeti ndani ya diary hiyo, nilichokuwa nimekihifadhi."Ndio alikuwa anaitwa Cosmas Siame. Huyu ni mtoto wake, ni yule mtoto aliyenusurika." Nilinong'ona. Nilijikuta nikipiga magoti na kusali. "Mungu, wewe ni mweza na hakuna kinachokushinda. Nimeamini baba kwamba kila jema tunalofanya ni akiba yetu ya kesho na kesho hiyo huanzia hapa duniani." Halafu nillinyamaza na kulia sana. Nililia kwa furaha na ugunduzi wa nguvu zinazomgusa binadamu kwa kila analofanya.Nilisimama nikiwa nimesawajika kabisa. Nilihisi kuwa mtu mwingine kabisa. Nilimfuata yule kijana na kumkumbatia huku nikiwa bado ninalia. "Mimi ni baba yako mdogo, ndiye nitakyekulea sasa. Ni zamu yangu sasa kukulea hadi mwisho" Naye alilia bila kujua sababu na alikuwa amechanganyikiwa kabisa. Nilirudi kwenye kiti na kumsimulia kilichotokea miaka 17 iliyopita.Tuliondoka hapo na kwenda kumwona shangazi yake Ubungo, eneo la maziwa ambako alikuwa amepanga chumba. Kutokana na hali yake nilimhamishia kwangu, baada ya kumsimulia kilichotokea. Huyo dada yake Cosmas alifurahi sana hadi akashindwa kuzungumza kwa saa nzima. Alifariki hata hivyo mwaka mmoja baadae, lakini akiwa ameridhika sana.Kijana Siame alisoma na kumaliza Chuo Kikuu na hivi sasa yuko nchini Australia anakofanya kazi. Ukweli ni kwamba ni mwanangu kabisa sasa. Naamini huko waliko Mbinguni wazazi wake wanafurahia kile walichokipanda miaka mingi sana nyuma. Lakini nami najiuliza bado. Ilikuwaje Cosmas akanipa msaada ule? Halafu najiuliza ni kitu gani kilimvuta mwanae Siame hadi ofisini kwangu akizipita ofisi nyingine zote? Nataka nikuambie, usiwe mbishi sana bila sababu, kuna nguvu za ziada zinazoongoza matokeo maishani mwetu....*************MWISHO*********** *********

SHARTI NI KUWA NDANI YA KRISTO

Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya(2 Wakorintho 5:17).

     Andiko hilo hapo juu ni tangazo la Mungu na ufunuo wa mtu mpya kupitia mtume Paulo. Hebu tuchambue huu mstari kwa uangalifu. Kwanza, unasema "mtu akiwa ndani ya Kristo..." ambayo inamaanisha "mtu yeyote," bila kujali ni nani, akishakuwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya. Mazingira ya mtu mpya ni Kristo. Angalia haijasema, "atakuwa kiumbe kipya" au "atakuja kuwa kiumbe kipya" bali, inasema '...amekuwa kiumbe kipya..." Hii siyo ahadi; ni tamko la uhalisia.
     Neno "ame..." ni kitenzi cha "sasa" , kinachoonesha jambo lililotokea sasa au uhalisia. Ikiwa u ndani ya Kristo, u kiumbe kipya SASA. Sio kwamba umetengenezwa upya, umebadilishwa, au umekarabatiwa; (bali) umezaliwa upya; (tena) bila kuwa na historia! Umebatizwa katika mwili wa Kristo, kwa Roho Mtakatifu( 1 Wakorintho 12:3). Haijalishi unahisi hilo au lah! Hiyo ndiyo picha yako kwa Mungu, hilo ndilo tamko Lake kuhusu wewe: u kiumbe kipya katika Kristo.
     Roho yako, kwa njia ya imani katika Kristo Yesu, imeumbwa upya, na sasa u mwenye haki wa Mungu ndani Yake.
     Na matokeo yake ni kuwa, sasa unaweza kusimama kwa ujasiri katika uwepo wa Mungu bila kujiona mwenye hatia, asiyejithamini au kujihukumu; sababu unao uzima na asili pamoja Naye; umezaliwa kwa Roho Wake( Yohana 3:6). 1 Yohana 4:17 inasema, "...jinsi Yeye Alivyo, ndivyo nasi tulivyo hapa ulimwenguni"; huendi kuwa kama Yeye, tayari umekuwa kama Yeye, na u ndani Yake, Naye yu ndani yako. Kwa pamoja, mu kiumbe cha ki-Ungu. Mungu na Abarikiwe.

    Ukiri
Mimi ni kiumbe kipya; ya kale yamepita, na mambo yote ni mapya kwangu! Mimi ni mrithi wa Mungu, na mrithi pamoja na Kristo. Nimekuwa huru na bila malipo nimepewa kibali cha kuwa uhalali kwa Mungu, kwa neema Yake ambayo nimetunukiwa katika Yesu Kristo. Utukufu wa kwa Mungu milele daima!.

Somo Zaidi:
Warumi 6:4 Basi tulizikwa pamoja Naye kwa njia ya ubatizo katika mauti Yake, kusudi kama Kristo Alivyofufuka kutoka katika wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

Wagalatia 3:27-29 Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo, hapana myahudi wala myunani. Mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawa sawa na ahadi.

Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu juu yao walio katika (ndani ya) Kristo Yesu.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
1 Petro 4
Ezekieli 33-34

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
Ufunuo 1:1-20
Hosea 3-4.

ROHO MTAKATIFU - MSAIDIZI WETU

ROHO MTAKATIFU-MSAIDIZI WETU MUHIMU!

Nami nitamuomba Baba, naye atawapa Msaidizi Mwingine, ili akae nanyi hata milele
    (Yohana 14:16)

   Roho Mtakatifu ni zawadi isiyo ya kawaida kwetu wana wa Mungu (Matendo 2:38). Yeye,kwa lugha ya komputa, ni kama "kishushio." Roho mtakatifu hutumika "kushusha"makabrasha ya kimbingu,na kuleta vitu vya kimbingu katika mfumo wa kibinadamu.
   Ndiye pekee, kwa mfano, akuwezeshaye kukubaliana na kuzaliwa kwa Yesu Kristo na bikira, kifo chake cha kujitoa,ufufuo wa ushindi na kupaa kwake kwa kitukufu kwenda mbinguni.Ni Roho mtakatifu pekee ndiye awezaye kukushawishi kuwa damu ya Yesu Kristo ilitosha kwa ajili ya wokovu wa binadamu wote. Hivyo unapoona ya kwamba unaelewa na unakubaliana na halisia hizi za kiroho inanaanisha kuwa Roho Mtakatifu amezifunua hizo kwako;anatenda kazi maishani mwako.
   Yesu alipowauliza wanafunzi wake, "Watu wanasema mimi ni nani? " Petro tu ndiye aliye jibu  kwa usahihi,naye alisema, "Wewe u Kristo,mwana wa Mungu aliye hai"(Mathayo 16:16). Jibu la Bwana kwa Petro lilikuwa, "Heri wewe Simion Bar-yona;kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni"(Mathayo 16:17).Petro hakuwa anakisia;inawezekana hakujua hili kichwani mwake;ufahamu wa kuwa Kristo ni nani uliwekwa ndani yake na Roho mtakatifu. Hakuna kipimo cha kibinadamu ambacho kinaweza kukuwezesha kuelewa Mambo ya kiroho.
    Hata katika kuhuiri na kuwahudumia wengine wokovu, unapaswa kuelewa kuwa Injili tuliyopewa, na kutakiwa kuipekeka katika mataifa ya ulimwengu,ni Injili ambayo haiwezi kueleweka na kufafanuliwa kibinadamu. Matokeo yake, ni kuwa tunahitaji Roho mtakatifu kuhudumu kwa kupitia sisi, na kutusaidia kuwapa uelewa wa ujumbe wale tunaowahudumia. Msaada ni muhimu katika kila tufantayo.
   Kamwe usijikute unafanya chochote au kujenga chochote kwa juhudi zako binafsi au kwa hekima ya kibinadamu;hakitafanikiwa. Zaburi 127:1 inasema, "Bwana asipoijenga nyumban waijengao wafanya kazi bure.."Yamkini u mtumishi wa Injili, usijalibu kulijenga kanisa kwa nguvu zako; usitegemee uwezo wako binafsi, kwa kuwa huo pekee hautasaidia.  Mtegemee Roho mtakatifu. Tumia huduma yake ya kitukufu katika maisha yako.  Yu ndani yako na hukusaidia kuishi maisha ya Ukristo ya ushindi na kuwa na mafanikio katika vyote ufanyavyo, kwa ajili ya utukufu wa Baba. Ndiye msaada wako wa muhimu!

     MAOMBI
Nakushukuru baba kwa kunijaza Roho mtakatifu, ambaye huendelea kumfunua Yesu Kristo kwangu, na kunipa uelewa katika mafumbo na siri za ufalme. Ninasaidiwa naye sana leo ili kuishi maisha ya ushindi katika Jina la Yesu. Amen.

Somo zaidi
matendo 1:8;1wakorinto 2:10-11;Yohane 14:16 AMP

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
1Petro 5
  Ezekieli 35-36
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKa 2
    Ufunuo 2:1-12
     Hosea 5-6.

Monday 24 November 2014

ZAWADI KUU TATU ZA MUNGU

ZAWADI KUU TATU ZA MUNGU.

Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa,kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utikufu wake na wema wake mwenyewe (2Petro 1:3).

   Kuna zawadi kuu tatu za Mungu katka Kristo Yesu tulizopewa kwa kupitia Injili.Nazo ni zawadi ya uzima wa milele,zawadi ya haki,na zawadi ya Roho Mtakatifu.
    
   Warumi 6:23 inatuambia"....bali karama ya Mungu ni Uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."Uzima wa milele ni uzima wa kiungu uliopewa ulipozaliwa mara ya pili. Uzima huu hauko sawa na uzima wa kibinadamu;ni uzima halisi wa Mungu. Huwezi kuufanyia kazi ili uupate uzima wa milele;huwezi kuupata kwa kulipia gharama yoyote;ni zawadi kutoka kwa Mungu. Bila uzima wa milele huwezi kuwa na asili sawa na ya Mungu; kusingekuwa na ushirika,hivyo kusingekuwa na uhusiano.
   Haki pia ni zawadi. Warumi 5:17 inasema, "...zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika Uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo." Haki ni asili ya Mungu ambayo inaezea usahihi wake:Ni asili yake na uwezo wa kuwa sahihi wakati. Huwa hakosei daima;na anapoweka asili hiyo na huo uwezo katika roho yako, ndipo unaweza kutembea sawa sawa na kusudi lake na kumpendeza katika maisha yako, nawe unaweza kusimama mbele zake bila kuwa na hisia zozote za kuhulumiwa,kutojithamini au kujiona mwenye makosa.
   Roho Mtakatifu pia ni zawadi ya za Mungu kwetu. Mtumie Mtumie Petro alisema katika Matendi 2:38,"Tubuni mkabatizwe kila Jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu."Roho Mtakatifu ni Mungu akitenda kazi ndani yetu. Kama Mkristo,unamhitaji Roho Mtakatifu ili uishi maisha ya ushindi katika Kristo. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu alisema, "Nami nitamuomba baba, naye atawapa msaidizi mwingine..."( Yohana 14:16)
   Roho Mtakatifu alikuja ili kukusaidia uishi maisha ya kikristo kwa sababu hakuna mtu wa kawaida awezaye kuishi maisha ya Ukristo.Roho Mtakatifu hukupatia uelewa wa neno la Mungu,hukuamsha katika Ubaba wa Mungu, na hudhihiriswa kusudi la Baba kwako na kupitia kwako. Roho Mtakatifu hukupa uwezo usio kifani wa kumtukuza Mungu na ujasiri wa kufanya Kristo afaamike katika ulimwengu wako.
  Zawadi hizi tatu ni muhimu sana kwetu kama wakristo,kwa sababu zinawakilisha utimizo wa mapenzi ya Mungu na kusudi la Yesu Kristo. Jifunze Neno na pia jifunze zaidi kuhusu hizo.

  UKIRI
Nakushukuru Bwana kwa kunibariki kwa zawadi za uzima wa milele, haki na Roho Mtakatifu! Kamba, hakika, zimeniangukia mahala pema,nami nina urithi mzuri. Sitahitaji kuhangaika kwa ajili ya jambo lolote jema maishani. Natambua zawadi za Mungu zitendazo kazi ndani yangu;najua ya kuwa nayaweza yote, kwa njia ya Kristo anitiaye nguvu. Haleluya!

Somo zaidi.
2wakorinto 1:21-22 Basi yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta ni Mungu. Naye ndiye aliye tutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.

Warumi 5:17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki watatawala katika uzima kwa yule mmoja Yesu Kristo.

1Yohane 5:11-12 Na huo ndio ushuhuda,ya kwamba Mungu alitupa alitipa uzima wa milele na uzima huo umo katika Mwanawe, yeye aliye naye Mwana,anao uzima wa asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
1petro 3
Ezekieli 31-32

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2.
Yuda1:12-25
Hosea 1-2

Sunday 23 November 2014

NI VEMA KUWA MWAMINIFU


Tazama, ataniua;sina tumaini;ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake (Ayubu 13:15).

   Tamko hilo hapo juu la imani na uadilifu linawakilisha uthibitisho wa imani ya Ayubu kwa Mungu huku akiwa katika changamoto za kutisha. Alikuwa katika mateso makubwa; hali yake ilizidi kuwa mbaya na ya kikatisha tamaa kiasi ambacho mke wake, kwa kebehi na hasira za mateso yake, akamwambia,"Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ukafe"(Ayubu 2:9).
  Lakini Ayubu,Biblia inasema, alishikilia imani yake na uadilifu katika Bwana, na hakumtenda Mungu dhambi. Hali yake haikumpelekea kufanya ukiri mbaya (Ayubu 2:10); inapendeza sana.
   Kisha katika Ayubu 13:15,licha ya ufahamu na maarifa yake hafifu kuhusu Mungu, alitoa tamko jingine la kustaajabisha,akisema,"Tazama, ataniua; sina tumaini; ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake." Mtazamo wa Ayubu unatufudisha kuwa haijalishi hali inakuwa mbaya kiasi gani, endelea kuliamini na kuwa mwadilifu katika Neno.  Kushikilia kwake imani na uadilifu kwa Mungu, Biblia inasema Mungu "akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake "/(Ayubu 42:12).
   Angalia pia uadilifu wa Petro na wanafunzi wengine ambao walichagua kubaki na Yesu wakati baadhi ya wanafunzi walipoudhika katika mafundisho yake na wakaacha kumfuata. Hawa wanafunzi waasi hawakijisikia vizuri kutokana na baadhi ya mambo waliyomsikia Yesu akiongea na wakajibu, "Neno hili ni gumu, ni nani awezaye,kulisikia?"(Yohana 6:60) Nao wakaondoka zao.
   Ndipo Yesu akawageikia Petro na wanafunzi wengine akawauliza,"Nanyi mwataka kwenda?"Petro akajibu, "Hapana Bwana.  Tu pamoja nawe daima, kwa kuwa tumeuamini ujumbe wako;tumekuamini ndiwe Kristo."
    Yeye na wanafunzi wengine wakabaki na Yesu.  Unajua nini? Kabla Yesu hajapaa, aliwaambia"nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi;mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israel "(Luka 22:29-30).
  Ni vizuri kuwa mwadilifu. Wakati Mambo yanapo onekana kuwa magumu na yenye kutatanisha,usijumuike na wale wanaotafuta njia nyingine. Bakia kuwa mwadilifu na muamini Mungu kubadili Mambo katika wakati muafaka.

   MAOMBI
Baba Mpendwa, Nakushukuru kwa kunipa moyo ulio mwadilifu,mwaminifu,na imara katika huduma yako na katika Neno lako. Haijalishi changamoto za kukatisha tamaa na ugumu wa mambo, naendelea kuto yumbishwa, nikiwa na ufahamu ya kwamba unayakamilisha yale yote yanayohusiana nami, katika Jina la Yesu, Amen.

Somo zaidi:
Wakolosai 3:23 Lo lote mfanyalo,lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu.

Hesabu 12:7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa:Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Petro 1:22-2:1-25
Ezekieli 29-30

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
Yuda1:1-11
Danieli11-12
Toa maoni yako kuhusu somo la leo katika :WWW.rhapsodyofrealities.org

Sunday 9 November 2014

AINA TATU ZA IMANI


Yakobo 2:14-26

UTANGULIZI
1.Imani ni kitu muhimu sana katika maisha ya mkristo.
a.Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Ebra 11:6
“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”
b.Mkristo anaokolewa kwa imani. Efeso 2:8
8Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
c.Mkristo anapaswa kuishi kwa imani. 2 Korintho 5:7

Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.

d.Jambo lolote tulifanyalo pasipo imani linaelezwa kuwa ni dhambi. Rumi 14:23
Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
2.Ni muhimu kutambua kuwa kuna aina tofauti za imani, lakini pamoja na hayo kuna imani moja tu ya kweli. “Imani iokoayo.”
3.Katika Yakobo 2:14-26 tunaona Yakobo akieleza aina tofauti za imani na anakazia kwenye imani itendayo kazi ya kuokoa roho.
(Tukianza na Yakobo 2:14-17 tunaona aina ya kwanza ya imani ambayo tunaweza kusema ni imani iliyokufa.)
14Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? 15Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? 17Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
AIMANI ILIYOKUFA (14-17)
IJINSI ILIVYO
1.Hubadili matendo kwa maneno.
a.Watu walio na imani hii huwa na sifa zifuatazo:
(1)Wanajua misamiati mizuri kwa maombi; pia wanajua mafundisho sahihi.
(2)Wanaweza kunukuu mistari ya Biblia kwa ufasaha zaidi.
b.Tatizo ni kwamba mwenendo wao hauendani na kile wanachokisema.
2.Imani hii ni imani ya ufahamu tu.
a.Iko kwenye mawazo ya mtu, mtu anajua mafundisho yote ya wokovu.
b.Lakini pamoja na kujua hayo mtu huyo hatii kile Mungu anachokiagiza wala hamtumainii Yesu katika wokovu wake.
c.Mkristo anaijua lakini haitendei kazi ile kweli.
IIJE IMANI HII INAWEZA KUOKOA?
1Hapana! Katika mistari mitatu Yakob 2: 17,20 na 26 Yakobo amesisitiza kuwa imani bila matendo imekufa.
2Tamko lolote la Imani lisiloleta mabadiliko katika maisha wala lisiloleta kazi njema ni tamko la uongo. Na hapo imani imekufa.
3Imani iliyokufa ni imani ya uongo inamwongoza mtu kwenye tumaini la uongo la uzima wa milele.
IIIJE TUNAYO IMANI ILIYOKUFA?
1Tunaweza kuwa nayo iwapo mwenendo wetu hauendani na maneno tunayosema.
2Tunaweza kuwa nayo iwapo kzi tuzifanyazo ziko kinyume na tunahubiri.
(Wapendwa yatupasa kuwa makini na imani ya kweny mawazo tu. Mana mtu mmoja alisema hakuna mtu ajaye kwa Yesu akawa kama alivyokuwa.)
Aina ya pili ya imani iliyoelezewa na yakobo ni…

BIMANI YA MASHETANI
IHata mashetani yanayo imani.
1Yanaamini katika Mungu(Si miungu bali ni Mungu)
2Yanaamini hata katika uungu wa Kristo. Mk 3:11-12
11Na pepo wachafu, kila walipomwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu. 12Akawakataza sana, wasimdhihirishe.
3.Si hivyo mapepo yanamini kuwepo na sehemu ya hukumu. Luka 8:31

Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.
4.Na zaidi mapepo yanaamini kuwa Yesu atakuwa Hakimu. Matayo 8:28-29

28Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. 29Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?

IIJINSI IMANI YA MASHETANI ILIVYO
Tumeona kuwa mtu mwenye imani iliyokufa huguswa kwenye ufahamu tu.
Mashetani yana guswa katika hisia zao. (kumbuka kuwa huamini na kutetemeka)
Hii imani iko juu zaidi ya imani iliyokufa. Inahusisha ufahamu na hisia.

IIIJE IMANI YA NAMNA HII INAWEZA KUOKOA?
1Hapana imani hii inaweza kuwemo ufahamuni mwa mtu na ikawemo moyoni mwake lakini mtu huyo akapotea milele.
2Imani ya kweli iokoayo inahusisha kitu zaidi, kitu zaidi ya kile kinachoweza kuonekana; mabadiliko katika maisha. Yakobo 2:18
18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
3Kuwa mkristo kunahusisha mambo mawili kumtumainia Kristo na kuishi kwa ajili ya Kristo.
a.Kwanza unapokea uzima.
b.Unadhihirisha uzima.

IVJE TUNAYO IMANI YA MASHETANI
1Tunaweza kuwa nayo iwapo tunaamini tu katika mambo sahihi na tunaishia kwenye hisia tu.
2Tunaweza kuwa na imani ya mashetani iwapo:
a.Kiufahamu tunakubali mafundisho sahihi.
b.Tunasisimuka kimazoea wakati wa ibada.
(Kwa hiyo Yakobo ameweka wazi kuwa aina hizi za imani kamwe haziwezi kuokoa; imani iliyokufa na imani ya mashetani. Yakobo pia akaendelea kuelezea kuhusu imani itendayo kazi ni imani pekee iokoayo.

CIMANI ITENDAYO KAZI (Yakobo 2:20-26)
20Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? 21Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? 22Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale. 23Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. 24Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake. 25Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? 26Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

AJE HII NI IMANI YA NAMNA GANI?

1Mahali pengine Biblia inatuambia kuwa imani msingi wake ni Neno la Mungu Rumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
2Imani itendayo kazi inamhusisha mtu mzima
a.Imani iliyokufa inahusisha ufahamu tu.
b.Imani ya mashetani inahusisha ufahamu na hisia.
c.Imani itendayo kazi inahusisha ufahamu, hisia na utashi.
(1)Ufahamu ni katika kuelewa kweli.
(2)Moyo ni kwa ajili ya shauku na kufurahi katika neno.
(3)Na utashi ni kwa ajili ya kutendea kazi kweli.
3Imani ya kweli, iokoayo huongoza kwenye matendo.
a.Si ya ufahamu tu.
b.Si ya hisia.
c.Ni imani itupelekayo kuwa na utii katika kufanya kazi njema.
BILI KUFAFANUA YAKOBO ANATUPA MFANO WA ABRAHAM NA RAHABU
1. Katika hawa tunaona kuwa:
a.Abraham alikuwa na baba wa wayahudi; Rahab alikuwa mmataifa.
b.Abrahamu alikuwa mcha Mungu; Rahabu alikuwa mwenye dhambi kahaba.
c.Abrahamu alikuwa rafiki wa Mungu lakini Rahabu alikuwa upande wa maadui wa Mungu.
2Je hawa wawili walikuwa na nini cha kuwafananisha? Wote walionyesha imani iokoayo kwa Mungu.
a.Abrahamu alionyesha imani yake kwa kazi zake. Yakobo 2:20-24
20Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? 21Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? 22Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale. 23Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. 24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.

b.Rahabu alionyesha imani yake kwa matendo yake. Yakobo 2:25-26
25Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? 26Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

3Kwa hiyo katika vifungu hivi tunajifunza kuwa:
a.Imani bila matendo imekufa. Yakobo 2: 20, 26
b.Imani peke yake haiwezi kumhesabia haki mtu. Yakobo 2:24
c.Imani kamilifu lazima iwe na matendo Yakobo 2:22
HITIMISHO
1Ni muhimu kila mwamini achunguze moyo na maisha yake na ahakikishe kuwa anayo imani iokoayo ambayo ni imani itendayo kazi.
2Shetani ni mdanganyifu mkuu na moja ya mbinu yake kuu ni kuiga…..
a.Anaweza kumshawishi mtu kuwa imani ya uongo ni ya kweli…na kwamba yule mtu anazo nguvu za kiroho.
3Yafuatayo ni maswali unayoweza kujiuliza katika kuichunguza imani yako.
a.Je kuna wakati nilijikugundua mwenyewe kuwa mimi ni mwenye dhambi na nikazikubali dhambi kwangu mwenyewe na kwa Mungu?
b.Je kuna wakati moyo wangu ulinisukuma niepuke ghadhabu ijayo. Je ni jitihada zipi nimefanya kuhusu dhambi zangu?
c.Je ni kweli naelewa injili kuwa kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zangu?
d.Je nilitubu dhambi kwa dhati na kuchukua uamuzi wa kuziacha? Je ninachukia dhambi na kumcha Mungu?
e.Je namtumania Kristo peke yake?
f.Je kuna mabadiliko katika maisha yangu? Je ninaendelea kutenda mema?
g.Je nina shauku ya kukua? Ninaweza kuwaambia wengine kuwa niko na Kristo?
h.Je ninafurahia ushirika na wapendwa?