Sunday 23 November 2014

NI VEMA KUWA MWAMINIFU


Tazama, ataniua;sina tumaini;ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake (Ayubu 13:15).

   Tamko hilo hapo juu la imani na uadilifu linawakilisha uthibitisho wa imani ya Ayubu kwa Mungu huku akiwa katika changamoto za kutisha. Alikuwa katika mateso makubwa; hali yake ilizidi kuwa mbaya na ya kikatisha tamaa kiasi ambacho mke wake, kwa kebehi na hasira za mateso yake, akamwambia,"Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ukafe"(Ayubu 2:9).
  Lakini Ayubu,Biblia inasema, alishikilia imani yake na uadilifu katika Bwana, na hakumtenda Mungu dhambi. Hali yake haikumpelekea kufanya ukiri mbaya (Ayubu 2:10); inapendeza sana.
   Kisha katika Ayubu 13:15,licha ya ufahamu na maarifa yake hafifu kuhusu Mungu, alitoa tamko jingine la kustaajabisha,akisema,"Tazama, ataniua; sina tumaini; ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake." Mtazamo wa Ayubu unatufudisha kuwa haijalishi hali inakuwa mbaya kiasi gani, endelea kuliamini na kuwa mwadilifu katika Neno.  Kushikilia kwake imani na uadilifu kwa Mungu, Biblia inasema Mungu "akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake "/(Ayubu 42:12).
   Angalia pia uadilifu wa Petro na wanafunzi wengine ambao walichagua kubaki na Yesu wakati baadhi ya wanafunzi walipoudhika katika mafundisho yake na wakaacha kumfuata. Hawa wanafunzi waasi hawakijisikia vizuri kutokana na baadhi ya mambo waliyomsikia Yesu akiongea na wakajibu, "Neno hili ni gumu, ni nani awezaye,kulisikia?"(Yohana 6:60) Nao wakaondoka zao.
   Ndipo Yesu akawageikia Petro na wanafunzi wengine akawauliza,"Nanyi mwataka kwenda?"Petro akajibu, "Hapana Bwana.  Tu pamoja nawe daima, kwa kuwa tumeuamini ujumbe wako;tumekuamini ndiwe Kristo."
    Yeye na wanafunzi wengine wakabaki na Yesu.  Unajua nini? Kabla Yesu hajapaa, aliwaambia"nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi;mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israel "(Luka 22:29-30).
  Ni vizuri kuwa mwadilifu. Wakati Mambo yanapo onekana kuwa magumu na yenye kutatanisha,usijumuike na wale wanaotafuta njia nyingine. Bakia kuwa mwadilifu na muamini Mungu kubadili Mambo katika wakati muafaka.

   MAOMBI
Baba Mpendwa, Nakushukuru kwa kunipa moyo ulio mwadilifu,mwaminifu,na imara katika huduma yako na katika Neno lako. Haijalishi changamoto za kukatisha tamaa na ugumu wa mambo, naendelea kuto yumbishwa, nikiwa na ufahamu ya kwamba unayakamilisha yale yote yanayohusiana nami, katika Jina la Yesu, Amen.

Somo zaidi:
Wakolosai 3:23 Lo lote mfanyalo,lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu.

Hesabu 12:7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa:Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Petro 1:22-2:1-25
Ezekieli 29-30

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
Yuda1:1-11
Danieli11-12
Toa maoni yako kuhusu somo la leo katika :WWW.rhapsodyofrealities.org

No comments:

Post a Comment