Thursday 27 November 2014

NGUVU YA KUTOA PEPO

Yesu Akamkemea, Akisema, fumba kinywa,  umtoke. Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka( Marko 1:25-26).

     Marko 16:17-18 inasema, "ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina Langu watatoa pepo...." Kila Mkristo anao uwezo wa kuwatoa pepo! Sio swala la kwamba "una nguvu" kiasi gani au jinsi gani upo "kiroho" ; cha muhimu ni kuwa Yesu Amekupa mamlaka Yake; unatembea katika jina Lake.
    Shetani hana haki ya kuendesha mambo katika maisha yako, au nyumbani mwako au katika maisha ya wale uwapendao. Tumia mamlaka yako katika Kristo dhidi yake.
     Unaweza kuwatoa pepo siku yoyote, muda wowote na mahala popote, kwa kutumia jina la Yesu tu. Usijadiliane naye; mtoe!
     Unaweza ukajiuliza. "Nitajuaje kuwa pepo ametoka ninapomkemea?" Hilo ni rahisi. Yesu Alisema, unapowaambia pepo watoke, hutoka. Neno Lake Linakamilisha hilo. Kazi yako ni kumkemea pepo atoke, na jukumu lake pepo ni kutii.
     Ingawa, wakati mwingine pepo hujionesha na kulia kwa sauti pindi wanapomtoka yule mtu unayewatoa kwake. Mfano ni kama tulivyosoma katika mstari wetu wa ufunguzi. Pia tunaona tukio kama hilo katika matendo 8:6-8 pale Filipo alipomuhubiri Kristo kwa watu: "...pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu..."
    Hivyo, katika kutoa pepo, roho waovu huweza kupiga yowe na kelele kwa kuteseka pindi wanapotoka; na kisha badiliko la wazi kwa wale ambao pepo wamewatoka hujionesha kuwa kuna tofauti.
     Hata hivyo, haijalishi pepo wamepiga yowe au kelele wakati ulipowakemea; cha muhimu ni kile Yesu Alichokisema,"...kwa jina Langu mtatoa pepo..."( Marko 16:17). Huo ndiyo uhalisia, na unapaswa kuwa ndiyo msingi wa imani yako. Hivyo, unapowakemea pepo, wanakuwa hawana chaguo lolote- zaidi ya kukimbia.

   Maombi
Baba Mpendwa, nakushukuru kwa mamlaka Uliyonipa ya kukemea pepo katika jina la Yesu. Shetani na wafuasi wake hawana nafasi katika nyumba yangu, mwili, kazi na kipato changu. Natumia mamlaka yangu katika Kristo kuwaweka pale wanapostahili- chini ya miguu yangu. Katika jina la Yesu. Amina.

Somo Zaidi:
Luka 10:18-19  Akawaambia, Nilimwona shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, Nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na ng'e, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.

Matendo 16:16-18  Ikawa tulipo kuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema watu hawa ni watumishi wa Mungu Aliye juu, wenye kuwahubiria Njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo Akakasirika, akageuka akamwambia yule pepo, nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yakobo 2-3:1-13
Ezekieli 20-21

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Yohana 4:14-21
Danieli 3-4.

No comments:

Post a Comment