Thursday 27 November 2014

ROHO MTAKATIFU - MSAIDIZI WETU

ROHO MTAKATIFU-MSAIDIZI WETU MUHIMU!

Nami nitamuomba Baba, naye atawapa Msaidizi Mwingine, ili akae nanyi hata milele
    (Yohana 14:16)

   Roho Mtakatifu ni zawadi isiyo ya kawaida kwetu wana wa Mungu (Matendo 2:38). Yeye,kwa lugha ya komputa, ni kama "kishushio." Roho mtakatifu hutumika "kushusha"makabrasha ya kimbingu,na kuleta vitu vya kimbingu katika mfumo wa kibinadamu.
   Ndiye pekee, kwa mfano, akuwezeshaye kukubaliana na kuzaliwa kwa Yesu Kristo na bikira, kifo chake cha kujitoa,ufufuo wa ushindi na kupaa kwake kwa kitukufu kwenda mbinguni.Ni Roho mtakatifu pekee ndiye awezaye kukushawishi kuwa damu ya Yesu Kristo ilitosha kwa ajili ya wokovu wa binadamu wote. Hivyo unapoona ya kwamba unaelewa na unakubaliana na halisia hizi za kiroho inanaanisha kuwa Roho Mtakatifu amezifunua hizo kwako;anatenda kazi maishani mwako.
   Yesu alipowauliza wanafunzi wake, "Watu wanasema mimi ni nani? " Petro tu ndiye aliye jibu  kwa usahihi,naye alisema, "Wewe u Kristo,mwana wa Mungu aliye hai"(Mathayo 16:16). Jibu la Bwana kwa Petro lilikuwa, "Heri wewe Simion Bar-yona;kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni"(Mathayo 16:17).Petro hakuwa anakisia;inawezekana hakujua hili kichwani mwake;ufahamu wa kuwa Kristo ni nani uliwekwa ndani yake na Roho mtakatifu. Hakuna kipimo cha kibinadamu ambacho kinaweza kukuwezesha kuelewa Mambo ya kiroho.
    Hata katika kuhuiri na kuwahudumia wengine wokovu, unapaswa kuelewa kuwa Injili tuliyopewa, na kutakiwa kuipekeka katika mataifa ya ulimwengu,ni Injili ambayo haiwezi kueleweka na kufafanuliwa kibinadamu. Matokeo yake, ni kuwa tunahitaji Roho mtakatifu kuhudumu kwa kupitia sisi, na kutusaidia kuwapa uelewa wa ujumbe wale tunaowahudumia. Msaada ni muhimu katika kila tufantayo.
   Kamwe usijikute unafanya chochote au kujenga chochote kwa juhudi zako binafsi au kwa hekima ya kibinadamu;hakitafanikiwa. Zaburi 127:1 inasema, "Bwana asipoijenga nyumban waijengao wafanya kazi bure.."Yamkini u mtumishi wa Injili, usijalibu kulijenga kanisa kwa nguvu zako; usitegemee uwezo wako binafsi, kwa kuwa huo pekee hautasaidia.  Mtegemee Roho mtakatifu. Tumia huduma yake ya kitukufu katika maisha yako.  Yu ndani yako na hukusaidia kuishi maisha ya Ukristo ya ushindi na kuwa na mafanikio katika vyote ufanyavyo, kwa ajili ya utukufu wa Baba. Ndiye msaada wako wa muhimu!

     MAOMBI
Nakushukuru baba kwa kunijaza Roho mtakatifu, ambaye huendelea kumfunua Yesu Kristo kwangu, na kunipa uelewa katika mafumbo na siri za ufalme. Ninasaidiwa naye sana leo ili kuishi maisha ya ushindi katika Jina la Yesu. Amen.

Somo zaidi
matendo 1:8;1wakorinto 2:10-11;Yohane 14:16 AMP

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
1Petro 5
  Ezekieli 35-36
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKa 2
    Ufunuo 2:1-12
     Hosea 5-6.

No comments:

Post a Comment