Kumekuwa na wimbi kubwa sana la waimbaji wakike wa nyimbo za
injili,kila siku kwa wastani kuna waimbaji kumi wapya kabisa wanatambulishwa
kwa njia mbalimbali aidha redioni,kwenye tv,magazetini,majaridani hata
mitandaoni.
Wimbi hili la ongezeko la waimbaji wa kike haliendani na
utoaji wa albamu. Katika hili kuna mijadala mbalimbali juu ya kwanini waimbaji
wa kike wengi hawatoi albamu zao na hizi ndio baadhi ya sababu zinazochangia:
-
Mtaji – Waimbaji wengi hawana pesa (mtaji) kwa
ajili ya kufanyia recordings ya nyimbo zao
-
Wito – Baadhi ya waimbaji hawana wito wa
kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji hivyo wanaimba tu kwa sababu wanajua
kuimba wakisahau kuwa uimbaji ni huduma moja wapo katika huduma za kumtumikia
Mungu na Mungu huwa hachezewi hivyo Mungu anaziba njia
-
Malengo – Kuna wengine wanaingia kwenye huduma
hii kwa kutamani tu bila kuwa na malengo
-
Tamaa – Pia tama za kimwili kwa waimbaji na
watengenezaji muziki (Producers) hupelekea kwa kukwamisha kazi kwa sababu
baadhi huingia kwenye mahusiano ya kingono kitu ambacho hupelekea kupoteza
concentration kwenye kazi pia dhambi huwa katikati yao.
-
Menejimenti – Waimbaji wengi hawana watu wa
kuwasaidia kusimamia kazi zao ili waweze kuzifanyikisha ziweze kuifikia jamii
kwa wakati muafaka.
HITIMISHO – Inahitajika kumuomba Mungu sana juu ya waimbaji
maana ndio huduma inayopigwa vita sana na Shetani.
Credits to @THE
BULLETS NEWS a whatsapp group
No comments:
Post a Comment