Thursday 27 November 2014

AINA MBILI ZA HATIMA

AINA MBILI ZA HATMA.

Na wale aliyowachagua tangu asili, hao Akawaita; na wale Aliowaita, hao Akawahesabia haki, hao Aliowahesabia haki Akawatukuza( Warumi 8:30)

     Kuna hatma mbili kwa kila mwanadamu. Kuna hatma ya kidunia na hatma ya KiUngu. Hatma ya kidunia huongozwa na vigezo kama vile familia uliyozaliwa, nchi uliyozaliwa, watu unaohusiana nao, taarifa unazozipokea au elimu n.k. Hayo yote yana matokeo katika hatma yako ya kidunia.
     Kwa mfano, kuna wale ambao ni matajiri, si kwa mafanikio yao wenyewe, bali kwa sababu ya familia walizozaliwa. Hiyo ndiyo hatma yao ya kidunia.
     Hatma ya kidunia hata hivyo, haiondoi kuhusika kwa mkono wa Mungu wa kiUngu wenye uweza; Ana uhusika wa ujumla katika ulimwengu. Ulimwengu ni mali yake. Lakini kuna baadhi katika ulimwengu huu ni viumbe wake, huku wengine ni wana wake. Analo kusudi jema kwa viumbe Wake wote- kila mmoja duniani- bali kipekee(maalumu) zaidi, Anayo hatma ya kiUngu kwa wana Wake- kila aliyezaliwa mara ya pili.
     Hatma ya kiUngu kwa kila mwanadamu huanza tu pindi anapozaliwa mara ya pili. Pale ndipo Mungu huwa Baba yako naye huanza kukuongoza. Pale ndipo Humtumtuma Roho Mtakatifu kuishi ndani yako na kukuongoza. Sasa Roho Mtakatifu huweka makazi ndani ya moyo wako.
    Wewe ni wa tofauti na ulimwengu. Kama Yesu Alivyosema katika Yohana 15:19, "...bali Mimi Nilliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia." Kila aliyezaliwa mara ya pili si wa ulimwegu huu. Umechaguliwa toka ulimwengu huu na Yesu. Ana alama zake kwako.
      Utajuaje kama mtu anatimiza hatma yake ya kidunia au ya kiUngu? Ni rahisi: nani hujitwalia utukufu katika maisha yake? Katika mambo afanyayo, ni nani hupokea heshima? Ni nani hupokea sifa? Ni nguvu ya nani inayomuwezesha kufanya afanyayo? Anaishi kwa ajili ya nani? Kama majibu yote yataonesha kuwa ni BWANA, basi hiyo ni hatma ya kiUngu, kwa mujibu wa biblia.

    Ukiri

Maisha yangu ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Nilizaliwa ili kumpa heshima, na kuonesha ubora Wake na ukamilifu katika ulimwengu huu. Hekima Yako, neema, na haki vinaonekana, kadri unavyodhihirisha ladha ya ujuzi Wako kupitia mimi kila mahali; hii ni hatma yangu: kuishi kwa ajili ya Yeye Aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.

Somo Zaidi:
2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.

Yeremia 1:5 Kabla sikakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Waefeso 1:11 Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawa sawa na kusudi Lake Yeye, Ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi Yake.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
1 Petro 1:1-21
Ezekieli 27-28

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
3 Yohana
Danieli 9-10.

No comments:

Post a Comment