Saturday 23 January 2016

UNAITWA,TUPA VAZI LAKO


MARKO 10;46-52
Inaelezea kulikuwa na Bartimayo kipofu alikuwa amekaa chini kando ya njia hajui maisha yake yatakuwaje,anavizia watu waje wamsaidie amekuwa ombaomba kwa miaka mingi kutokana na upofu wake,inawezekana nawe una upofu wa ndani umeteseka kwa jambo Fulani kwa miaka mingi hujui utatokaje hapo ktk magumu yako..YESU alipopita Bartimayo hakulaza damu akaanza kupaza sauti akimwita YESU...
Mstari 48-50. Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu.Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita.AKATUPA VAZI
LAKE, akaruka, akamwendea..
Bartimayo aliposikia YESU anamwita AKALITUPA VAZI LAKE,vazi lililokuwa linamtambulisha kama yeye ni ombaomba,lile vazi ndilo lililompa chakula,lilimfunika na kumtambulisha yeye ni kipofu na anahitaji msaada lakini Bartimayo alipoitwa na YESU alilitupa hakujali watu wakija km wakimuona hana vazi lile watamsaidiaje,yeye alisikia sauti ya watu inayompa matumaini JIPE MOYO,INUKA,ANAKUITA,kuitwa kwake kulimpa matumaini kuwa atapata vazi lingine si la kuomba tena,leo watumishi tunakuita uje kwa YESU wewe uliyevaa vazi la umalaya inawezekana hilo vazi la uchangudoa ndilo linalokupa chakula nawe unaketi kando ya njia kusubiri wanaume wapite na tena umelivaa nusu uchi ili kuwatamanisha wanaume,unafikiri kama nikilivua nitakula wapi?basi Jipe moyo utapata chakula toka kwake aliyesema njooni kwangu nyinyi mnasumbuka na kuelemewa na mizigo,wacha kuwa na maswali,wewe inuka mpelekee mizigo yako utoke ktk uchafu wako huyo anaekuita atakupa chakula.Kuna watu wengine kwakuwa wao wamevikwa mavazi ya UKIMWI basi wanavizia watu watakaojipendekeza kwao nao wawavike hayo mavazi ya UKIMWI ili wafe wote,..Kuweni makini wana wa MUNGU msipoongozwa na ROHO MTAKATIFU nanyi mtavishwa mavazi na wakuu wa giza yenye gharama kubwa hadi yaje kuvuka umepoteza utu wako na kutumia gharama kubwa sana kuyavua.Wewe Unalalamika ndoa ngumu kumbe wewe mwenyewe umejivika vazi la michepuko ukilitupa hilo vazi ndoa itakuwa nzuri..Na wewe uliyevaa vazi la utapeli,uongo,uzinzi,usengenyaji,usikubali kuwa hivyo jumapili ya leo YESU anakuita inakupasa ulitupe na kumfuata .Bartimayo alipoitwa na YESU alilitupa vazi lake nawe litupe hilo vazi..Wengine wakiingia kanisani wanalivua wakionekana watakatifu wakitoka nje wanalikumbuka vazi lake na kulivaa tena..Basi ukimwendea YESU mpe udhaifu wako kuwa sitaki kulivaa tena,maana YEYE ALICHUKUA MADHAIFU YETU,KAMA UKILITUPA NA KULICHUKIA,NAYE YESU ATAKUPA ROHO YA UWEZESHO ILI USILIVAE TENA..Atakupa vazi jeupe safi la utakatifu UFUNUO 3;4-5 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa MAVAZI MEUPE, kwa kuwa wamestahili.Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima...
AMEN.

No comments:

Post a Comment