Monday 24 November 2014

ZAWADI KUU TATU ZA MUNGU

ZAWADI KUU TATU ZA MUNGU.

Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa,kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utikufu wake na wema wake mwenyewe (2Petro 1:3).

   Kuna zawadi kuu tatu za Mungu katka Kristo Yesu tulizopewa kwa kupitia Injili.Nazo ni zawadi ya uzima wa milele,zawadi ya haki,na zawadi ya Roho Mtakatifu.
    
   Warumi 6:23 inatuambia"....bali karama ya Mungu ni Uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."Uzima wa milele ni uzima wa kiungu uliopewa ulipozaliwa mara ya pili. Uzima huu hauko sawa na uzima wa kibinadamu;ni uzima halisi wa Mungu. Huwezi kuufanyia kazi ili uupate uzima wa milele;huwezi kuupata kwa kulipia gharama yoyote;ni zawadi kutoka kwa Mungu. Bila uzima wa milele huwezi kuwa na asili sawa na ya Mungu; kusingekuwa na ushirika,hivyo kusingekuwa na uhusiano.
   Haki pia ni zawadi. Warumi 5:17 inasema, "...zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika Uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo." Haki ni asili ya Mungu ambayo inaezea usahihi wake:Ni asili yake na uwezo wa kuwa sahihi wakati. Huwa hakosei daima;na anapoweka asili hiyo na huo uwezo katika roho yako, ndipo unaweza kutembea sawa sawa na kusudi lake na kumpendeza katika maisha yako, nawe unaweza kusimama mbele zake bila kuwa na hisia zozote za kuhulumiwa,kutojithamini au kujiona mwenye makosa.
   Roho Mtakatifu pia ni zawadi ya za Mungu kwetu. Mtumie Mtumie Petro alisema katika Matendi 2:38,"Tubuni mkabatizwe kila Jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu."Roho Mtakatifu ni Mungu akitenda kazi ndani yetu. Kama Mkristo,unamhitaji Roho Mtakatifu ili uishi maisha ya ushindi katika Kristo. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu alisema, "Nami nitamuomba baba, naye atawapa msaidizi mwingine..."( Yohana 14:16)
   Roho Mtakatifu alikuja ili kukusaidia uishi maisha ya kikristo kwa sababu hakuna mtu wa kawaida awezaye kuishi maisha ya Ukristo.Roho Mtakatifu hukupatia uelewa wa neno la Mungu,hukuamsha katika Ubaba wa Mungu, na hudhihiriswa kusudi la Baba kwako na kupitia kwako. Roho Mtakatifu hukupa uwezo usio kifani wa kumtukuza Mungu na ujasiri wa kufanya Kristo afaamike katika ulimwengu wako.
  Zawadi hizi tatu ni muhimu sana kwetu kama wakristo,kwa sababu zinawakilisha utimizo wa mapenzi ya Mungu na kusudi la Yesu Kristo. Jifunze Neno na pia jifunze zaidi kuhusu hizo.

  UKIRI
Nakushukuru Bwana kwa kunibariki kwa zawadi za uzima wa milele, haki na Roho Mtakatifu! Kamba, hakika, zimeniangukia mahala pema,nami nina urithi mzuri. Sitahitaji kuhangaika kwa ajili ya jambo lolote jema maishani. Natambua zawadi za Mungu zitendazo kazi ndani yangu;najua ya kuwa nayaweza yote, kwa njia ya Kristo anitiaye nguvu. Haleluya!

Somo zaidi.
2wakorinto 1:21-22 Basi yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta ni Mungu. Naye ndiye aliye tutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.

Warumi 5:17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki watatawala katika uzima kwa yule mmoja Yesu Kristo.

1Yohane 5:11-12 Na huo ndio ushuhuda,ya kwamba Mungu alitupa alitipa uzima wa milele na uzima huo umo katika Mwanawe, yeye aliye naye Mwana,anao uzima wa asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
1petro 3
Ezekieli 31-32

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2.
Yuda1:12-25
Hosea 1-2

No comments:

Post a Comment