Thursday 27 November 2014

SHARTI NI KUWA NDANI YA KRISTO

Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya(2 Wakorintho 5:17).

     Andiko hilo hapo juu ni tangazo la Mungu na ufunuo wa mtu mpya kupitia mtume Paulo. Hebu tuchambue huu mstari kwa uangalifu. Kwanza, unasema "mtu akiwa ndani ya Kristo..." ambayo inamaanisha "mtu yeyote," bila kujali ni nani, akishakuwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya. Mazingira ya mtu mpya ni Kristo. Angalia haijasema, "atakuwa kiumbe kipya" au "atakuja kuwa kiumbe kipya" bali, inasema '...amekuwa kiumbe kipya..." Hii siyo ahadi; ni tamko la uhalisia.
     Neno "ame..." ni kitenzi cha "sasa" , kinachoonesha jambo lililotokea sasa au uhalisia. Ikiwa u ndani ya Kristo, u kiumbe kipya SASA. Sio kwamba umetengenezwa upya, umebadilishwa, au umekarabatiwa; (bali) umezaliwa upya; (tena) bila kuwa na historia! Umebatizwa katika mwili wa Kristo, kwa Roho Mtakatifu( 1 Wakorintho 12:3). Haijalishi unahisi hilo au lah! Hiyo ndiyo picha yako kwa Mungu, hilo ndilo tamko Lake kuhusu wewe: u kiumbe kipya katika Kristo.
     Roho yako, kwa njia ya imani katika Kristo Yesu, imeumbwa upya, na sasa u mwenye haki wa Mungu ndani Yake.
     Na matokeo yake ni kuwa, sasa unaweza kusimama kwa ujasiri katika uwepo wa Mungu bila kujiona mwenye hatia, asiyejithamini au kujihukumu; sababu unao uzima na asili pamoja Naye; umezaliwa kwa Roho Wake( Yohana 3:6). 1 Yohana 4:17 inasema, "...jinsi Yeye Alivyo, ndivyo nasi tulivyo hapa ulimwenguni"; huendi kuwa kama Yeye, tayari umekuwa kama Yeye, na u ndani Yake, Naye yu ndani yako. Kwa pamoja, mu kiumbe cha ki-Ungu. Mungu na Abarikiwe.

    Ukiri
Mimi ni kiumbe kipya; ya kale yamepita, na mambo yote ni mapya kwangu! Mimi ni mrithi wa Mungu, na mrithi pamoja na Kristo. Nimekuwa huru na bila malipo nimepewa kibali cha kuwa uhalali kwa Mungu, kwa neema Yake ambayo nimetunukiwa katika Yesu Kristo. Utukufu wa kwa Mungu milele daima!.

Somo Zaidi:
Warumi 6:4 Basi tulizikwa pamoja Naye kwa njia ya ubatizo katika mauti Yake, kusudi kama Kristo Alivyofufuka kutoka katika wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

Wagalatia 3:27-29 Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo, hapana myahudi wala myunani. Mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawa sawa na ahadi.

Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu juu yao walio katika (ndani ya) Kristo Yesu.

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
1 Petro 4
Ezekieli 33-34

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
Ufunuo 1:1-20
Hosea 3-4.

No comments:

Post a Comment